Mambo 8 ambayo si rahisi kujua kwenye simu za Samsung Galaxy - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mambo 8 ambayo si rahisi kujua kwenye simu za Samsung Galaxy

0
Sambaza

Matumizi ya simu yamekuwa ni kitu cha kawaida sana siku hizi na kadri siku zinavyozidi kusogea idadi ya wanaomiliki simu janja inazidi kupanda ila wangapi tunachunguza simu zetu kuweza kujua menginenyo ambayo yanahitaji akili zaidikuyajua?

Katika simu janja ambazo zinafanya vizuri sokoni na kuleta ushindani katika soko la biashara za simu ulimwenguni simu za Samsung Galaxy ni mojawapo kutokana na mengi mazuri ambayo simu hizo yanayo. Katika kuperuzi kwangu kama mdau wa teknolojia nikakumbana na buy flagyl over the counter Mambo yasijulikana na wengi katika simu za Samsung Galaxy.

Fahamu vitu 8 unavyoweza kufanya kwenye simu za Samsung Galaxy.

Samsung ambao kila toleo wanalotoa linakuwa ni la kuvutia zaidi kuzidi toleo lililopita katika simu za Samsung Galaxy unaweza ukafanya yafuatayo:-

 • http://msdubindesign.com/tag/ma/ Kupiga order estrace cream screenshot kwa kutumia kiganja cha mkono. Katika simu janja nyingi ukitaka kupiga screenshot basi ni lazima ushikilie cha kuzimia simu na kitufe cha kupunguzia sauti kwa pamoja ndio uweze kupiga picha ya ukurasa wa mbele kwenye simu yako. Kwenye simu za famili ya Samsung Galaxy cha kufanya ni kupitisha kiganja cha mkono wako mbele ya simu yako.

Hata hivyo kuweza kufanikisha jambo hilo utatakiwa kufanya settings kidogo:

 • GS3: Settings > Motion > Palm swipe to capture (under Hand motions)
 • GS4: Settings > My device > Motions and gestures > Palm motion > Capture screen
 • Galaxy Note 3: Settings > Controls > Palm motion > Capture screen
 • GS5, GS6/GS6 Edge, Note 4, Note Edge: Settings > Motions and gestures > Palm swipe to capture.

  Pangusa kwa kiganja upige screenshot

 • Kutumia simu yako kiurahisi zaidi’ (Easy mode). Una apps ambazo unazitumia mara kwa mara? Ukiweka simu yako (Samsung Galaxy) katika mfumo wa Easy Mode inachofanya ni kusogeza zile apps ambazo wengi hupenda kuzitumia pamoja na apps nyingine utakazopenda zijumuishwe tena zikionekana kwa maandishi yanayosomeka vilivyo.

Hata hivyo kuweza kufanikisha jambo hilo utatakiwa kufanya settings kidogo:

 • GS3: Settings > Home screen mode > Easy mode
 • GS4: Settings > My device > Home screen mode > Easy mode
 • Galaxy Note 3: Settings > Device > Easy mode
 • GS5, GS6/GS6 Edge, Galaxy Note 4/Note Edge: Settings > Easy mode

Kama simu janja yako ipo katika mfumo wa Easy Mode utaweza kuzifikia zile apps ambazo zinapendwa kutumia na wengi kwa haraka zaidi.

 • Kufunga simu kwa kutumia alma ya kidole (fingerprint). Simu nyingi imezoeleka kuwa na mfumo wa kutumia nenosiri au kuchoro umbo fulani ili kuweza kufungua na kutumia kwa sababu za kiusalama zaidi lakini katika simu janja nyingi za hali ya juu zimekuwa zikija na mfumo wa kufungua simu yako kwa kutumia alama za kidole.

Hata hivyo kuweza kufanikisha jambo hilo utatakiwa kufanya settings kidogo:

 • GS5, Galaxy Note 4/Note Edge: Settings > Finger Scanner
 • GS6/GS6 Edge: Settings > Lock screen and security > Fingerprints

Alama za vidole kwenye simu za familia ya Samsung Galaxy zinaweza zikakuwezesha kutumia fingerprint kuweza kuingia kwenye akaunti yako ya Samsung au kuhakiki kwenye akaunti yako ya Pay Pal kabla ya kufanya malipo.

 • Uwezo wa kutumia simu yako hata kama umevaa gloves. Katika mikoa ya baridi kama Arusha, Mbeya, Kilimanjaro kuona mtu amevaa baridi alfajiri au hata jioni si jambo la kushangaza kwa mikoa hiyo kutokana na hali ya hewa ya huko. Sasa simu za Samsung Galaxy unaweza ukatumia simu yako bila shida yoyote hata kama ukiwa umevaa gloves.

Hata hivyo kuweza kufanikisha jambo hilo utatakiwa kufanya settings kidogo:

 • GS4: Settings > My device > Display > High touch sensitivity
 • Galaxy Note 3: Settings > Controls > Increase touch sensitivity
 • GS5, Galaxy Note 4 / Note Edge: Settings > Display > Increase touch sensitivity

Kwa kupangusa vidole vyako viwili kwa kwenda chini itakuwezesha kufungua ukurasa wa Settings haraka zaidi na ifahamike kuwa itakuwa ni changamoto kutumia simu yako aina ya iPhone ukiwa umevaa gloves.

 • Find my mobile. Ile changamoto ya kuibiwa simu na kupoteza matumaini ya kuipatra simu yako inaweza ikawa historia kama utakuwa umeweka settings vizuri ili kuweza kujua mahali simu yako ilipo.

Hata hivyo kuweza kufanikisha jambo hilo utatakiwa kufanya settings kidogo:

 • GS3: Settings > Security > Remote controls
 • GS4: Settings > More > Security > Device administrators > Android Device Manager
 • GS5: Settings > Security > Device administrators > Android Device Manager
 • GS6/S6 Edge: Settings > Lock screen and security > Find My Mobile
 • Galaxy Note 3: Settings > General > Security > Device administrators > Android Device Manager
 • Galaxy Note 4/Note Edge: Settings > Security > Remote controls

Kuweza kufanya Find My Mobile ifanye kazi inabidi uwe na akaunti ya Samsung na pia uingie (login).

Soma pia: App ya Find My iPhone ilivyosaidia kupatikana simu zaidi ya 100

 • Kutumia apps mbili kwa wakati mmoja. Ndio, inawezekana kabisa kuweza kutumia programu tumishi mbili tofauti kwa wakati mmoja; yaani kioo cha simu kinakuwa kimejigawa mara mbili: kila upande ukifanya kulingana na kazi ya app husika.

Hata hivyo kuweza kufanikisha jambo hilo utatakiwa kufanya settings kidogo:

 • GS3: Settings > Display > Multi window
 • GS4: Settings > My device > Display > Multi window
 • GS5, Galaxy Note 4/Note Edge: Settings > Multi window
 • Galaxy Note 3: Settings > Device > Multi window

  Unaweza ukaamuru simu yako aina ya Samsung Galaxy kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja kwa kuwenda sehemu ya menu ndogo inayoonekana baada ya kupangusa kioo kwa kwenda chini.

 • Matumizi ya sahihi/sauti au sura yako kufungua simu. Kama hutaki kutumia nenosiri, pattern au fingerprint kufungua sim uako basi unaweza uatumia sura yako/sauti au sahihi yako kuweza kufungua simu yako na kuitumia.

Hata hivyo kuweza kufanikisha jambo hilo utatakiwa kufanya settings kidogo:

 • GS3: Settings > Lock screen > Screen lock > Face unlock
 • GS4: Settings > My device > Lock screen > Screen lock > Face unlock
 • Galaxy Note: Settings > Security > Screen lock > Face unlock.
 • Galaxy Note II: Settings > Lock screen > Screen lock > Face unlock

Kuiamuru simu yako ifungnuke kwa kutumia sauti yako unatakiwa ushikilie alama ya kipaza sauti na utaamke maneno kwa sauti inayolingana.

Kwenye Samsung Note 3 inaruhusu kufungua simu yako kwa kutumia mfumo wa sahihi yako na ni lazima usaini kwa kutumia peni iliyokuja na simu.

 • Kuzima/kuwaka baada ya muda fulani. Mahali ambapo jicho lako linaangalia wakati fulani linaweza likaamua kuzima/kuwasha kwa muda kulingana na wapi unapoangalia; kwa kutumia kamera ya mbele kama umeiangalia simu yako kwa sekunde kadhaa basi itaendelea kuwaka na pindi tu itakapogunduahuangalii tena pale baada ya muda fulani ambao utakuwa umeshauweka kwenye miapngilio basi itazima kwa muda.

Hata hivyo kuweza kufanikisha jambo hilo utatakiwa kufanya settings kidogo:

 • GS3, GS5, Galaxy Note 4/Note Edge, GS6/GS6 Edge: Settings > Display > Smart stay
 • GS4: Settings > My device > Smart screen > Smart stay
 • Galaxy Note 3: Settings > Controls > Smart screen > Smart stay

Kamera ya mbele na jicho ndio kiini katika kuwezesha simu yako kuwaka/kuzima kwa muda.

Tuambie, wewe ulikuwa unajua vingapi kabla ya uchambuzi huu? Unadhani sasa umeshawishika kumiliki simu aina ya Samsung Galaxy?

Vyazno: Mashable, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Vodacom na wizi wa fedha mtandaoni
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.