TWITTER: Mamia Ya Wafanyakazi Katika Hatihati Ya Kupoteza Kazi Zao!

0
Sambaza

Twitter inaweza ikapunguza wafanyakazi wake kwa kiasi kikubwa sana, wafanya kazi wa ndani ambao wanaijua taarifa hiyo wamedokeza kuwa inawezekana kazi 300 zikapunguzwa.

buy valtrex online europe

buy Depakote 250mg tablets Nguvu kazi ya Twitter  inaweza ikaathirika kwa asilimia 8 kama hili likitokea. Unaweza ukajiuliza ni kwanini haya yote yanatokea lakini ukweli ni kwamba kampuni linafanya vibaya siku hizi katika maswala mazima ya kifedha.

Mtu Akitembea Mbele Ya Nembo Ya Twitter

Licha ya fedha tuu twitter vile vile imeshindwa kujipanua na kuongeza watumiaji wengi zaidi na pia taarifa zingine zilizotoka kwamba kampuni hilo linataka kujiuza lakini mpaka sasa hajajitokeza mnunuzi.

Mmiliki wa Twitter pia anamiliki makampuni mengine yanayojitegemea na hili limewafanya watu kuanza kujiuliza maswali kama ni kweli anaweza kuendesha makampuni yote hayo na kuhakikisha kuwa anapata matokeo chanya (twitter iko mbioni kumshinda).

Ufuto Wenye Nembo Ya Twitter Ukionyesha Unawafuta Mtu (Mfanyakazi)

Kumbuka watu wote ambao hapo mwanzo waliweka nia ya kuinunua kampuni ya twitter (Salesforce, Alphabet, Walt Disney) wote walijitoa katika mchakato huo.

INAYOHUSIANA  Slack imeboresha kitu na kuzidi kuvutia

Kama kazi hizi zilikuwa hazina umuhimu mkubwa kuzipunguza ni jambo zuri. Ukiachana na hilo pia kama kazi nyingi zinaweza zikafanywa na mtu mmoja basi ni vizuri pia. Hii itawasaidia Twitter hata kukusanya faida kubwa kidogo ukilinganisha na mwanzo.

Ningependa kuona mawazo yako na wewe, naomba niandikie hapo chini sehemu ya comment ni nini mtazamo wako.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.