Marekani; Simu za Samsung Galaxy Note 7 zote hazirusiwi kwenye ndege

1
Sambaza

Mamlaka ya usafiri wa anga nchi Marekani imepiga marufuku kwa msafiri yoyote kuingia na simu janja aina ya Samsung Galaxy Note 7 kwenye ndege kwa sababu zinahatarisha maisha.

Samsung galaxy note 7 zote

Samsung galaxy note 7

Kutokana na kesi mbalimbali kuhusu kulipuka kwa simu aina ya Samsung Galaxy Note 7 iliyotoka miezi michache iliyopita idara ya usafirishaji nchini Marekani ilitangaza kuwa simu haziruhisiwi kuingia kwenye ndege.

Awali mamlaka ya anga nchini Marekani ilisema kuwa simu zote zizimwe abiria wanapoingia kwenye ndege.

Marekani peke yake imeripotiwa jumla ya kesi 96 za betri za Samsung kulipuka zikiwemo kesi 23 mpya kabisa tangu Sept, 15. Huku Samsung iliripotiwa kesi 13 zilizohusisha kuunga vitu, kesi 47 zilizosababisha uharibifu wa mali kutokana na simu hizo kulipuka.

Note 7

Mamlaka hiyo imesema kuwa iwapo mhudumu wa kwenye ndege akigundua kuwa kuna mtu mwenye simu hiyo basi mtu huyo aamuriwe kuizima simu hiyo na assitumie kabisa.

SOMA PIA:  Zanzibar kuzima mitambo ya Analogia kwenda Digitali Agosti 31, 2017

Ni muhimu mtu yoyte mwenye kutumia simu aina ya Samsung galaxy note 7 basi ahakikishe kuwa hatumii simu hiyo kabisa ili kuepuka kupata madhara ya yenye mwenye kuungua au mali zake mbalimbali kuungua.

TeknoKona inajali wasomaji wake ndio maana tumewaambia hili. Tupe maoni yako na endelea kutufuatilia popote pale ulipo.

Vyanzo: USA Today, tovuti mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com