Jumla ya masaa bilioni 1 ya video hutazamwa YouTube kila siku!

1
Sambaza

Upo hapo? Google watoa taarifa rasmi inayoonesha ukuaji wa utumiaji wa tovuti maarufu kwa masuala ya video. Jumla ya masaa bilioni 1 ya video hutazamwa YouTube kila siku duniani kote.

Je unaona ni idadi ndogo? – Fahamu ya kwamba kama wewe pekee yako ukikaa na kutazama video kwa muda wa masaa bilioni 1 itakuchukua zaidi ya miaka 110,000 kumaliza video hizo.

bilioni 1 ya video

Mtandao wa YouTube unazidi kuwa maarufu na unaendelea kukua kwa kasi huku ukizidi kutafuna pesa nyingi za matangazo kutoka makampuni mbalimbali yanayoona kutangaza YouTube kuna ufanisi mkubwa ukilinganisha na kuweka matangazo kwenye stesheni mbalimbali za Televisheni.

SOMA PIA:  Mambo 10 ya ujanja ujanja unayoweza kufanya kwenye iPhone 6/iPhone 6+

Idadi hii ya video kutazamwa kwa siku ilifikiwa mwishoni mwa mwaka jana na wanategemea ata mwaka huu ukuaji utakuwa mkubwa tuu. Kuelewa jinsi mtandao huo unakua kwa kasi angalia data hizi:

airtel tanzania bando

  • Mwaka 2014 ndio kwa mara ya kwanza mtandao huo ulifikisha rekodi ya idadi ya masaa milioni 300 ya kutazamwa video kwa siku kwenye mtandao huo
  • Mwaka 2015 ndio utazamaji wa video za jumla ya masaa milioni 500 kwa siku ilifikiwa
SOMA PIA:  Ifahamu Program Endeshaji Mpya Ya Android Baada Ya 'Android Nougat!

Na sasa 2016 wamefanikiwa kufikisha bilioni 1 – hapa unaona kuna ukuaji mkubwa kweli kweli unaendelea.

Je na wewe ni mtumiaji mkubwa wa mtandao wa YouTube? Je utumiaji wako umeanza kuwa mkubwa zaidi kuanzia mwaka gani?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com