MASTODON:Ufahamu mtandao mbadala wa Twitter unaokuja kwa kasi

0
Sambaza

Mastodon ni mtandao unaofanana kwa karibu zaidi na Twitter na unazidi kusambaa kwa kasi, siku za hivi karibuni umezidi kupata umaarufu hasa baadhi ya watumiaji nguli wa Twitter kuanza kuupigia upatu huku baadhi wakiuponda kwamba hautafikia mahali Twitter imeweza kufikia.

mastodon

Hii ndio logo ya mtandao huu.

Je ni kweli huu mtandao unafanana na Twitter?

Kimuundo  mtandao huu unafanana na mtandao wa Twitter kwasababu ni kweli mtandao huu kama ulivyo Twitter unafanya kazi kwa kuruhusu mtumiaji kuchapisha machapisho madogo madogo kwa wingi yaani kwa kimombo Micro blogging. 

Pia Mastodon inatumia karibu kila kionjo ambacho kinatumiwa katika Twitter ingawa vingi vimepewa majina tofauti, wakati Tweet ikiitwa Toot, Retweet ikiitwa Boost, like katika mtandao huu imeitwa Favorite.

Kwa upande wa umbopande ( 🙂  😀 kiswahili cha profile ) la mtumiaji na namna ambavyo watumiaji wanaathiriana mitandao hii miwili inamfanano mkubwa.

mastodon

Muonekano wa timeline katika mastodon.

Je Mastodon inatofautiana nini na Twitter?

Mtandao huu mpya tofauti na Twitter wenyewe umeundwa katika programu huru, hii inamaana kwamba mtu yeyote anaruhusa ya kuitafiti, kuisambaza ama kuibadili programu hiyo ya Mastodon.

Twitter wao ndio wapanga na kuamua mabadiliko bila ya uamuzi wa moja kwa moja wa mtumiaji mfano waliamua kwamba kitufe cha Favorite kibadilishwe kuwa Like na alama yake ya nyota ikabadilishwa kuwa alama ya moyo, katika mfumo wa programu huru hakuna hili yaani mmiliki wa Mastodon hawezi kubadili mfumo au muundo wa mtandao huu.

SOMA PIA:  Mtoto wa miaka 10 kutengeneza roboti itakayokuwa ikifurahisha jiji la Paris

Kwa lugha nyepesi ni kwamba mtandao huu utaendeshwa vile ambavyo watumiaji wenyewe wangependa uendeshwe na sio ma bwana wakubwa huko Silcon Valley.

Je nani atafanya maboresho na mabadiliko ya msingi katika mtandao huu?!

Mastodon inaundwa na mitandao midogo midogo mingi (ambayo inaitwa Instances), kila mtandao mdogo unautawala wake binafsi na sheria zake na kama mnauwezo wa kuandika programu basi mnaweza kufanya mabadiliko ya kimuundo na kuufanya mtandao uwe vile mnapenda.

SOMA PIA:  VW yajipanga kuhamia katika utengenezaji wa magari yanayotumia umeme

Kuunda mtandao mdogo ndani ya Mastodon unahitaji tu kuwa na server ama kupangisha huduma hiyo na kisha kuendesha programu huria ya Mastodon.

Je Mastodon inawezakuwa mbadala wa Twitter?!

Ukweli ni kwamba bado mapema saana kujua kama Mastodon kweli inaweza kuja kuwa mbadala wa Twitter, ingawa matumani ni makubwa lakini bado mtandao huu mpya unasafari ndefu sio tu kuibadili twitter ila hata kufikia mahali twitter imefika.

Endelea kufuatilia ukurasa wako wa Teknokona na tutakuletea makala zaidi juu ya mtandao huu wa Mastodon ili ujue jinsi ya kuutumia. – https://mastodon.social/

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com