fbpx

Matangazo kwenye simu: Jinsi ya kuzuia matangazo kwenye simu za Android

1

Sambaza

Katika moja ya maswali ambayo kwa zaidi ya miaka miwili tumekuwa tukiulizwa ni kwa namna gani mtu anaweza akazuia kabisa matangazo yasijitokeze anapoperuzi kupitia simu rununu.

Limekuwa jambo la karaha na wakati mwingine kufedhehesha pale unapoperuzi ukijaribu kutafuta hiki na kile mtandaoni au umefungua app fulani na ghafla tu unaona tangazo kuhusu kitu fulani mele ya uso wa simu yako; more tips here ni kitu ambacho kwa maoni yangu kinapoteza umakini wa kile ulichokuwa unakifanya kabla ya tangazo hilo kujitokeza.

Lakini je, kwanini matangazo hayo hujitokeza?

Kwa wasiofahamu basi mfahamu leo kwamba tangazo lolote linalojitokeza bila ya kutarajia au linabadilika badilika ni matangazo yaliyo chini ya Google (Google Ads) kwa mantinki ya kumuingizia kipato yule ambaye tangazo hilo limejitokeza kwenye tovuti yake.

Matangazo yanayojitoza yamekuwa yakiingiza kipato lakini ni chanzo cha mapato kilicho na changamoto sana.

Wakati mwingine yule anayetangaza ile biashara yake huwa analipa kiasi fulani cha pesa ili basi tangazo lake liweze kuonekana mara nyingi, bidhaa yake kuweza kujitangaza vyema na hatimae kufahamika hitisho likiwa ni kupata wateja.

Mbinu za kutumia ili kuzuia matangazo kwenye simu janja.

 1. http://theborrowedboutiqueblog.com/tag/the-posh-society/instagram.com/theborrowedboutique Tumia kivinjari cha Opera Mini. Moja ya sifa kuu kuhusu kivinjari cha Opera Mini ni kuwa na uwezo wa kuzuia matangazo yanayojitokeza tu; uwezo huo upo ndani kwa ndani ya kivinjari cha Opera Mini. BOFYA HAPA kujua undani na uwezo wa Opera Mini kuzuia matangazo kwenye simu janja.

  Kivinjari cha Opera Mini kinasifika kwa kuwa na wepesi wa kuvungua tovuti pale pale mtu anapoperuzi kupitia kivinjari hicho.

 2. Tumia Ad-Block Browser. Hiki ni kivinjari kinachopatikana kwenye soko la programu tumishi kwa wanatumia Android hivyo kinaweza kuwa mbadala wa kivinjari kwa dhumuni kuu la kuondokana na kadhia ya matangazo yasiyokuwa na mpangilio wowote.

  Ad-Blck kama jina lake lilivyo maana yake ni kivinjari kinachozuia matangazo kwenye simu. Ukiwa unatumia kivjari hiki sahau kabisa kuhusu kuona matangazo yakitokeza ghafla ghafla.

 3. Mpangilio (settings) kwenye kivinjari cha Google Chrome. Kupitia kivinjari cha Chrome pia inawezekana kabisa ukazuia matangazo ambayo yanatokea tu bila yeye kufahamu. Kitu cha kufanya mi kuingia kwenye Settings>>Site settings>>Pop-ups, kisha unachagua Blocked.

  Kivinjari cha Chrome kina wapenzi wengi lakini kama usipozuia matangazo ya kujitokeza tokeza basi utakuwa unaendelea kupata kadhia hiyo.

 4. Tumia Data Saver Mode kwenye kivinjari cha Chrome. Kinjari cha Chrome kina njia ya pili ya kuweza kupambana na matangazo yanayotokea tu bila ufahamu pale mtu anapoperuzi. Pia kwa kufanya kipengele cha Data Saver kuwa wazi (on) basi utapunguza utumiaji mkubwa wa kifurushi cha intaneti na kufanya kivinjari kuperuzi kwa kasi na kumfanya mtu akifirahie.

  Kufanya Data Saver kuwa wazi unafungua kivinjari cha Chrome>>Settings>>Data Saver kisha unaweka on.

   

INAYOHUSIANA  Amazon kuunda programu ya kujipima nguo

Ingawa makala hii imeangazia zaidi kwa upande wa simu za Android lakini baadhi ya mbinu zilizoelezwa hapo juu ni mtambuka kwa maana ya kwamba kuweza kusaidia kwa wanaotumia mfumo endeshi wa iOS kwenye vifaa vyao.

Ningependa kusikia maoni yake je, makala hii inakusaidia kuondokana na tatizo la matangazo yanayojitokeza kwenye simu? Niandikie hapo chini na endelea kufuatilia TeknoKona kila siku.

Vyanzo: Tech Advisor, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|