Jiandae kwa Matangazo ndani ya Facebook Messenger

0
Sambaza

Lengo la kuzidi kuongeza mapato ndani ya kampuni ya Facebook kumeleta uamuzi wa kuleta matangazo ndani ya Facebook Messenger.

Huduma ya kuchati inayopatikana ndani ya app ya Messenger kutoka mtandao maarufu wa Facebook inaletewa matangazi ndani yake.

App ya Facebook Messenger ni moja ya app inayotumika zaidi duniani na uamuzi huu wengi wanauona sio mzuri ata kidogo. Inasemekana tayari matangazo ndani ya app hiyo yameanza kuonekana kwa baadhi ya watumiaji na inategemewa muda si mrefu yatasambaa kwa watumiaji wengine wote duniani kote.

SOMA PIA:  Jinsi ya kufuta kabisa akaunti ya WhatsApp

Matangazo haya yatakuwa katikati ya orodha ya maongezi yako na watu wengine. Na ingawa utaweza kuondoa tangazo usilolipenda hakuna namna ya kusitisha matangazo katika app hiyo.

Matangazo ndani ya Facebook Messenger

Matangazo ndani ya Facebook Messenger

Wengi wanaona Facebook wameingilia eneo la faragha kidogo, na wanaamini kwa uamuzi huu basi watu wasishangae sana kama muda si mrefu matangazo yataletwa kwenye app nyingine maarufu ya kuchati inayomilikiwa na Facebook – yaani WhatsApp.

Vipi je wewe umepokeaje habari hizi? Je ni mtumiaji mkubwa wa app ya Messenger?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com