Pengine kwa sababu moja au nyingine yupo mtu ambaye usingependa aone picha unazoweka instagram? Instagram imekuwa inapata umaarufu zaidi hasa hapa kwetu kwa siku za hivi karibuni watu wengi wamejiunga na katika hali ya kawaida siyo kila aliyejiunga ungependa aone picha zako kwa hiyo hapa nitakuonesha jinsi ya kumblock mtu instagram.
- Lazima ujue jina analotumia mtu unayetaka kumblock katika instagram,
- Nenda katika sehemu ya kutafuta (search) kama inavyooneshwa katka picha hapo chini
- Tafuta akaunti unayotaka kuiblock
4. Ifungue akaunti hiyo na ubaki katika ukurasa mkuu.
5. Nenda katika menyu kuu ( hii ni sehemu iliyo juu kulia ambapo kuna vidoti vitatu)
6. Chagua Block User, chaguo ambalo ndilo litaifungia akaunti hiyo isiweze kuona picha zako na pia kuweka maoni.
7. Thibitisha chaguo lako. Katika hatua hii unaweza kukubali ama kukataa kumzuia mtu, kumbuka kama ukikubali hapa basi huyo mtu atakuwa amezuiwa.
Baada ya hapo akaunti hii uliyo iblock haitaweza kuona picha ama kuweka maoni katika picha yako yeyote, hii hutumiwa hasa kuwazuia watu wanaoweka vitu visivyo kupendeza katika sehemu za maoni ya picha zako, ama watu ambao hutaki kabisa waone yale unayoweka katika akaunti yako!
No Comment! Be the first one.