Memoji: App ya kuzifanya picha zako kuwa emoji.

0
Sambaza

Memoji ni app ambayo kama zilivyo app nyingine za picha inaongeza manjonjo katika picha zako, lakini jipya katika Memoji ni uwezo wake wa kufanya sura za watu katika picha kuwa kama emoji.

Memoji

Muonekano wa baadhi ya picha ambazo zimegeuzwa katika emoji tofauti tofauti kwa kutumia memoji.

Ni wazi kwamba zama tunazoishi sasa ni zama za picha, tunapiga picha nyingi na pia tunasambaza picha nyingi zaidi katika mtandao kwa siku kushinda nyakati nyingine zozote za huko nyuma jambo hili linafanya watengenezeaji wa App kujikita katika app zinazohusiana na picha zaidi.

SOMA PIA:  Jinsi Ya Ku'Log Out' Instagram Kwa Kutumia Kifaa Kingine!

Memoji imejipatia umaarufu mkubwa tangu kuachiwa kwake kwasababu ndiyo app ya pekee ya mtindo huu inayopatika katika soko kwa sasa.

App hii inakupa uwezo wa kupiga picha na kisha kuibadili kuwa GIF ya emoji inayokupendeza ( kwa  sasa emoji ambazo unaweza kutumia ni  emoji tisa tu. Unaweza kupiga picha kwa kutumia app hii kwaajiri ya kuzigeuza kuwa emoji lakini pia unaweza kuchukua picha kutoka katika maktaba ya simu yako.

memoji

Muonekano wa app hiyo ukiwa unachagua emoji ya kutumia.

Kwa sasa app hii ipo kwa watumiaji wa iPhone tu lakini kwa jinsi ilivyopokelewa vizuri ni wazi kwamba siku za hivi karibuni itawafikia na watumiaji wa simu za Android na nyinginezo. Picha ulizotengeneza kwa app hii unaweza kuzisambaza katika app nyingine kama vile WhatsApp, Twitter na Instagram, ama pia unaweza kuzihifadhi katika simu yako.

SOMA PIA:  BBM300: Gari hili spesheli linafyatua matofali 300 kwa dakika! #Teknolojia

Kama bado haujaijaribu hii app hebu ijaribu na utuambie kama hizi kelele ilizopata mtandaoni kweli inazistahili ama ndio yale yale ya promo?.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com