Facebook yaleta Messenger kwa ajili ya watoto chini ya umri wa miaka 13

Facebook yaleta Messenger kwa ajili ya watoto chini ya umri wa miaka 13

1
Sambaza

Facebook imeamua kutanua wigo wa biashara na kuleta app ya kufanya mazungumzo kwa njia ya maandishi mahususi kwa watoto ambao wana umri kuanzia miaka 13 kurudi chini.

Sote tunafahamu na asilimia kubwa ya watu wanatumia Facebook Messenger iliyojaa mengi mazuri na uhuru zaidi lakini katika kuwafanya wazazi wajue mazungumzo ya watoto wao kwenye mtandao wa kijamii maarufu duniani wa Facebook, Facebook imeamua kuja na Messenger Kids.

Messenger Kids inawezesha wazazi kuzungumza na watoto wao kwa njia ya maandishi kupitia Messenger. Pia watoto wanaweza kuchati na marafiki zao kwa marafiki ambao wazazi wamewakubali.

Kilichopo kwenye app ya Messenger Kids.

order metformin 850 >Inafahamika kabisa kuwa ili uweze kutumia Messenger basi ni lazima uwe na akaunti ya Facebook na ni hivyo hivyo kwenye hii app mpya kutoka Facebook lakini ikiwa na tofauti kidogo; http://healthynaturalchanges.com/2015/10 akaunti ya Facebook itakayokuwa inatumika ni ile ya mzazi, mtoto hataweza kutengeneza akaunti yake mwenyewe ili kutumia app ya Messenger Kids.

http://ourdiyhouse.com/tag/fancy-drill-bits/ >Kwenye Messenger Kids Facebook hawataonyesha matangazo kwenye hiyo app wala kukusanya taarifa zao hao watoto ila imeweka wazi kuwa itakuwa inachukua baadhi ya taarifa ambazo ni muhimu kwa Facebook.

Messenger Kids: App mahususi kwa watoto chini ya miaka 13 kuweza kuchati na marafiki zao pamoja na wazazi/mlezi.

>Facebook haitawahamishia watoto hao kwenye Messenger ya wakubawa pale watakapokuwa wamefikia umri za zaidi ya miaka kumi na tatu lakini inaweza ikawaruhusu watoto hao kuhamishia namba za simu za marafiki zao kwenye Messenger Kids.

Kwa mujibu wa sheria ya kimataifa makampuni yanayomiliki mitandao ya kijamii haayruhusiwi kuruhusu mtoto aliye chini ya umri wa miaka 13 kuwa na akaunti kwenye Facebook, Twitter, Instagram, n.k.

Jinsi ya kutumia Messenger Kids.

>Hatua ya kwanza kabisa ni kupakua app ya Messenger Kids kwenye simu janja/tabiti ya mtoto wako. Kisha ni kutoa mamlaka fulani kwenye kifaa cha mtoto wako (simu janja/tabiti) kwa kutumia barua pepe/namba ya simu pamoja na neno siri ileile unayotumia kuingia kwenye akaunti yako ya Facebook. Hatua hii haitengeneza akaunti ya Facebook ya mwanao/kumpa uwezo wa kutumia akunti yako.

INAYOHUSIANA  TTCL na vifurushi vya usiku

>Utatengeneza profile ya mtoto wako (kwa ajili ya kuchati tu) kwa kuweka jina la mtoto wako kupitia kwenye akaunti ya mzazi ya Facebook kwenye app ya Messenger Kids. Baada ya hapo unaweza ukamrudishia mtoto simu/tabiti yake na kwa kila ombi la urafiki litakalotumwa mzazi ndio atakayekuwa na uwezo wa kuidhinisha ombi hilo la urafiki.

Kupitia app kuu ya Facebook mzazi atakuwa na uwezo wa kuona maombi yote ya urafiki kwenda kwa mtoto baada ya kuweka mpangilio kwenye Messenger Kids.

Messenger Kids: Hatua kwa hatua namna ya kutengeneza akaunti kwenye app ya Messenger Kids.

Messenger Kids imezinduliwa 2017 Dec 4 na kwa sasa inapatikanac kwenye  iPhone, iPad and iPod Touch na kwa Android na tabiti za Amazon inatarajiwa kupatikana baadae kidogo. Haya wazazi tupe maoni yenu kuhusu app ya Messenger Kids.

Vyanzo: The guardian, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|