Miaka 30 ya mafaili ya mtindo wa GIF. - Fahamu historia yake! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Miaka 30 ya mafaili ya mtindo wa GIF. – Fahamu historia yake!

1
Sambaza

Mwezi huu video fupi ambazo zinatumika katika mitandao ya kijamii maarufu kama GIF zimetimiza miaka 30 tangu zianzishwe, GIF ambazo zinatumika zaidi kama meme kwa sasa zilianza kutumika mwaka 1987.

Seroquel cheap mexican

where can i buy erythromycin gel via GIPHY

Prozac GIF ambayo mwanzoni zilitumika kama mfumo wa mafaili ambao unaweza kusomeka katika kompyuta tofauti tofauti zimebadilika saana, makala hii pamoja na yote itakuletea mambo kumi ambayo pegine ulikuwa huyajui juu ya mfumo huu wa mafaili.

Nani aligundua mfumo huu wa mafaili!?

via GIPHY

Mfumo huu ulitengenezwa na mwandishi wa software anayeitwa Steve Wilhite, Steve alikuwa anafanya kazi katika kampuni ya watoa huduma za intanet  inayoitwa CompuServe.

Mfumo huu ulitengenezwa kwa lengo gani?

Wakati akianzisha mfumo huu Steve alikua anatafuta njia ambayo watumiaji wa intanet wangeweza kuona na kushusha mafaili ya picha, Compuserve walihitaji mfumo ambao utawezesha mteja kuona na kushusha mafaili kutoka katika kompyuta ya aina yeyote ile (Kumbuka miaka hiyo kompyuta zilikuwa zinatofautiana sana mfumo wa uendeshaji kutegemea na kampuni zilizotengeneza kompyuta).

Neno GIF linatamkwaje hasa!?

Kumekuwa na ubishi mkubwa wa namna neno GIF linavyo tamkwa, wapo ambao wanasema inatamkwa kama vile inavyoandikwa yaani GIF lakini walikuwepo ambao walisema inatamkwa kwa kuanza na herufi Ji yaani JiF(u). Steve alipoulizwa alisema GIF inatamkwa kwa kuanza na herufi Ji hivyo kwa mujibu wa muanzilishi inatamkwa JIF(u),  😀  😀  😀 najua wengi mlikua mnaitamka tofauti.

Lini ilianza kutumika katika mitandao ya kijamii.

GIF zimekuwa zikitumika katika baadhi ya mitandao ya kijamii kama vile Reddit kwa muda mrefu lakini katika mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter imechelewa saana kuanza kutumika. Facebook walianza kuruhusu GIF mwaka 2015 ambao walifuatiwa na mitandao mingine kama Twitter na WhatsApp.

GIF ilianza kabla ya mtandao.

Wakati mfumo huu unaanza bado mtandao ama World Wide Web ulikua bado haujaanza kutumika, WWW ilianza kutumika mwaka 1991 miaka 4 baada ya GIF kuanza kutumika.

GIF iliwahi kupotea baada ya teknolojia ya flash na HTML5 kupata umaarufu kwa waandika programu za kompyuta.

Mfumo wa mafaili wa GIF haujawa na safari tulivu, kunakipindi Flash na HTML5  zilikua maarufu sana kiasi GIF ikawa kama inataka kupotea lakini kwa bahati nzuri mwaka 2012 meme zikaja na GIF ikawa ni kama imefufuka.

mafaili mtindo wa gif

Inasemwa kwamba GIF ilifufuka katika michezo ya Olimpiki ya majira ya joto 2012

Michezo ya majira ya joto ya Olimpiki ya mwaka 2012 ndio hasa chimbuko la GIF kama meme ama tunaweza sema katika michezo hii ndipo hasa GIF zilianza kutumika kama meme. Katika kipindi hiki ndipo neno GIF lilipoingia katika kamusi ya KIngereza ya Oxford.

GIF zinatumika wapi hasa?

Toka mwaka 2012 GIF zinatumika zaidi katika mitandao ya kijamii na mtandao kiujumla, watumiaji wengi wa GIF wanatumia mfumo huu kuwakilisha hisia zao katika mfumo wa video fupi zinazojirudia. Mfano badala ya kutumia maneno kumwambia mtu unampenda unaweza tumia GIF

Unaweza kupata wapi GIF?

Mtandao wa GIPHY unayo akiba kubwa ya GIF mbali mbali kwaajiri ya jumbe tofauti, na kama unataka GIF kwa matumizi ndani ya mitandao kama Twitter GIF zipo moja kwamoja (hata kwa WhatsApp) unachotakiwa ni kutafuta unayotaka kuitumia.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo pengine ulikuwa hauyajui kuhusu GIF, naamini makala hii itakuwa imekuongezea jambo fulani. Mfumo huu wa mafaili unaonekana hautakufa leo ama kesho na pia ni moja kati ya vitu vinavyochangamsha mitandao ya kijamii. Karibu kutufuata katika kurasa zetu za Facebook Twitter na Instagram kwa habari za teknolojia katika lugha yako ya kiswahili.

via GIPHY

Facebook Comments

Sambaza
Share.