Ujio wa Microsoft Apps. Ikiwa inaonesha jinsi gani Microsoft wametambua umuhimu wa simu na tableti zinazotumia Android katika kukuza utumiaji wa apps zake kampuni hiyo imekuja na soko la apps za Microsoft.
Ukipakua app yao ya soko la apps zao basi utaweza kupakua apps mbalimbali zinazotoka kwao kwa urahisi zaidi. Soko hilo limekuja kwa jina la Microsoft Apps na tayari linapatikana katika soko la apps la Google Play.
Kwa sasa apps mbalimbali kama vile Skype na zile za Microsoft Office zinapatikana humo, Microsoft wamesema watazidi kuongeza apps zaidi.
Unaweza pakua soko hilo la Microsoft Apps hapa -> Microsoft Apps | Google Play
No Comment! Be the first one.