Microsoft wanataka kompyuta ziwe na sehemu ya laini ya simu

0
Sambaza

Kuwezesha intaneti kwenye kompyuta nyingi itakulazimu kupata huduma hiyo kupitia njia ya WiFi au kuchomeka waya wa intaneti, Microsoft wanataka kurahisisha mambo.

Microsoft wanataka kompyuta ziwe na sehemu ya laini ya simu ndani yake

Microsoft wanataka kompyuta ziwe na sehemu ya laini ya simu ndani yake. Na tayari wanachukua hatua kuliwezesha hilo.

Alhamisi iliyopita katika kutaniko la watengenezaji vifaa vya elektroniki nchini China, Microsoft wametoa taarifa rasmi ya kwamba wanafanya maboresho katika programu endeshaji yao (Windows 10) kuruhusu uwezo wa kutumia laini kwa ajili ya huduma ya intaneti ndani ya vifaa kama vile laptop na ata kompyuta za ‘desktop’.

SOMA PIA:  Ripoti TCRA: Idadi ya watumiaji wa Intaneti yaongezeka Kufikia milioni 23

Uwezo huo utawezesha pia hadi kwenye tablet zinazotumia programu za Windows. Pia kutakuwa na kiapp kitakachokusaidia kupanga vizuri utumiaji wako wa data.

Inategemewa kwa mataifa yaliyoendelea Microsoft wanaweza kutengeneza mfumo wa kutoa laini spesheli ambazo watakuwa wamekubaliana na mitandao ya simu kwa wateja wao kununua vifurushi spesheli kwa ajili ya intaneti ya kutumia kwenye kompyuta hizo. Kwa jinsi wenyewe Microsoft wanataka kwa sasa ni kuwa na laini zisizoweza kutolewa ila tunategemea watengenezaji wanaweza pingana na hilo na hivyo kutengeneza eneo la kuweka laini linaloweza chomoka na mtumiaji kubadilisha laini.

SOMA PIA:  Maboresho: Huduma ya Google Photos yazidi boreshwa

http://candacenkoth.com/?q=tadalafil-citrate-bulk-powder Je watengenezaji kompyuta wataanza kufanya hivyo hivi karibuni? Tutaendelea kufuatilia muendelezo wa jambo hili.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com