Microsoft Waipiga Chini Windows Media Center ktk Windows 10

1
Sambaza

Kama tulivyoona mabadiliko mengi yanazidi kuonekana yatakuwepo ndani ya toleo lijalo la programu endeshaji ya Windows kutoka Microsoft. Baada ya kutangaza kuachana na programu ya Internet Explorer na kuja na Microsoft Edge (Soma – Microsoft Edge: Kivinjari Kipya) sasa wametangaza pia kuachana na programu ya Windows Media Center.

Windows Media Center ni programu inayosaidia kutumia na kupanga mafaili kama vile muziki, filamu, na picha kwa urahisi sana na wengi walipenda kutumia programu hii pale walipokuwa wanaunganisha kompyuta yao na TV, yaani kutumia kioo cha TV kama vile za Samsung na zingenezo pale wanapotaka kuangalia filamu/muvi n.k

Programu hii ilikuwa inajumuishwa ndani ya programu endeshaji za Windows Vista na Windows 7, ila walipoleta Windows 8 hawakuijumuisha moja kwa moja bali walikupa uwezo wa kuishusha kupitia kuinunua kwa dola 10 za kimarekani kutoka kwenye soko la apps/programu la Windows.

Muonekano wa Programu hiyo ikiwa inatumika

Muonekano wa Programu hiyo ikiwa inatumika

Hivyo kama ulikuwa unaipenda programu hii fahamu hutaweza ipata kwenye toleo la Windows 10, ata kama kompyuta ilikuwa na programu hii alafu ukachagua kusasisha (upgrade) kwenda Windows 10 kupitia mtandao basi programu hii itaondolewa na hivyo kukosekana katika Windows 10.

SOMA PIA:  Apple yapata pigo baada ya taarifa kuhusu bidhaa zake kuvuja

Je kuna mabadiliko yapi ya Windows 10 yamekuvutia zaidi? Kama bado hufahamu mambo mbalimbali kuhusu toleo hili la Windows linalokuja hivi karibuni basi BOFYA HAPA -> WINDOWS 10 upate kusoma makala yetu kuhusu programu endeshaji hii.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com