Microsoft yashinda kesi dhidi ya Serikali ya Marekani

0
Sambaza

Mahakama ya rufani nchini Marekani imesema kuwa Microsoft haiwezi kulazimishwa kutoa taarifa kutoka kwenye barua pepe ya mtumiaji ambazo zimehifadhiwa nje ya Marekani.

Shirika linalojihusisha na masuala ya kitteknolojia

Shirika linalojihusisha na masuala ya kiteknolojia.

Baada ya kupigania haki ya kutotoa taarifa mbalimbali za wateja wao Microsoft imeshinda kesi hiyo dhidi ya Marekani iliyofunguliwa mwaka 2013. Kesi hiyo ilimhusisha mtu mmoja ambaye anadaiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya hivyo Marekani ilikuwa ikitaka iruhusiwe kuweza kuangalia barua pepe pamoja na data nyingine za mtu huyo.

Microsoft ilikataa kutoa data za mtu huyo kutokana na taarifa zake kuhifadhiwa katika servers zilizoki Dublin, Ireland hivyo hawana haki ya kupata taarifa za mtu yeyote kutokana na server hizo kuwa nje(overseas) ya Marekani.

Kwa mujibu wa sheria za Marekani mahakama haziruhusiwi kutoka idhini ya kuruhusu mamlaka husika kutoa data za mtu na kupewa mamlaka nyingine kama data hizo zimehifadhiwa nje ya nchi.

Inaaminika kuwa Marekani ndio nchi ya kwanza kushinda rufani kuhusu kutoa data mtu ambazo zimehifadhiwa nje ya Marekani. Dhumuni la rufani hiyo na sio kwa faida ya Marekani tu ni kama wangeruhusiwa kuweza kuzuia/kupekua taarifa za mtu hata kama data hizo zimehifadhiwa nje ya nchi husika.

Kompyuta zenye kasi zaidi na zenye uwezo wa kuhifadhi kiasi kikuwa cha data-Severs

Servers-Kompyuta zenye kasi zaidi na zenye uwezo wa kuhifadhi kiasi kikuwa cha data.

Makampuni mengi yanajihusisha na teknolojia yamekuwa yakiweka severs zao overseas, Ireland ikiwa ndio nchi inayoongoza kuwa na severs nyingi kutoka nje ya nchi hiyo kutokana na kutotoza ushuru mkubwa na pia hali ya hewa ya nchi ni rafiki kwa vitu vya kielekronki kama servers.

SOMA PIA:  Apple wataka simu zao ziwe na uwezo wa kuwa laptop kamili! #Teknolojia

Microsoft kama kampuni imepokea ushindi huo kwa furaha sana na kuwa kama chachu ya wao pamoja na makampuni mengine kuweka servers zao nje ya nchi na kufanya data za wateja wao kuwa salama na kutokuwa na ruhusu ya data hizo kupekuliwa.

Vyanzo: Tech Times, BBC

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com