MiniTool Power Data Recovery: Programu ya kuokoa data zilizofutwa au kupotea

0
Sambaza

Kuna mara nyingi unaweza kujikuta umefuta mafaili kwa bahati mbaya, au ata yanaweza yakawa yameliwa na programu za uharibifu kama vile Virusi n.k.

Ukiwa katika hali hii mara nyingi ni muhimu kujua na kuwa na programu za kukuwezesha kuzipata data zako zilizopotea. Na leo tunakufahamisha kuhusu programu ya MiniTool Power Data Recovery.

minitool data recovery

Muonekano wa programu ya MiniTool Data Recovery

Programu hii inayopatikana kwa toleo la bure na la kuuzwa, inakuwezesha kuyapata mafaili yaliyopotea au kufutwa bahati mbaya kwenye;

  • Hard drives za kompyuta
  • USB Flash Drive
  • diski zingine kama vile CD/DVD.
SOMA PIA:  Mac Pro iliyoboreshwa na yenye nguvu zaidi kutoka Apple

Ingawa programu hii itakusaidia kupata mafaili hayo si mara zote utaweza kuyapata katika hali ya kuweza kutumika tena – mfano kama yameharibiwa vibaya zaidi na virusi n.k.

Vya kuzingatia ukitumia programu hii

Usipakue (install) programu hii kwenye diski uhifadhi ambayo ndio unataka kujaribu kuokoa data kutoka huko. Yaani kwa mfano kama data zako zilipotea wakati zilikuwa kwenye diski C basi install programu hii kwenye diski D.

MiniTool Data Recovery inafanya kazi Windows na Mac pia.

Utumiaji

Ukishapakua programu hii na kuifungua utakutana na muonekano wa kawaida unaokupa moja kwa moja maelezo ya kwa urahisi kabisa kuhusu ni kitu gani unataka kufanikisha, mfano kama ni kuokoa mafaili yaliyofutwa bahati mbaya (Undelete Recovery), au kuokoa data katika diski iliyopoteza data (Damaged Partition Recovery), na pia kuna kuokoa hadi data kutoka CD/DVD n.k.

SOMA PIA:  Backup and Sync: App/Programu Mpya ya Google Drive yaja

MiniTool Power Data Recovery itafanya utafutati wa mafaili kutoka diski uliyochagua na kisha kukuwekea orodha yake vizuri kabisa. Pia utaweza kuwa na uwezo wa kuchagua matokeo kwa aina ya mafaili unayotaka mfano PDF, n.k.

Programu hii inapatikana kwa utumiaji wa bure kabisa kwa kuokoa kiasi cha data cha hadi GB 1 na ni ya kulipia kwa uokoaji wa kiwango kikubwa cha data zaidi ya hapo.

Leseni ya toleo linalouzwa ni takribani zaidi ya 150,000/= na hii inaonekana ni muhimu kwa watu wenye utumiaji mkubwa wa njia mbalimbali za uhifadhi data na kama huwa kuna uhitaji wa mara nyingi wa kuokoa data.

SOMA PIA:  Marekani: Programu ya Antivirus ya Kaspersky Lab marufuku serikalini

Je wewe huwa unatumia njia gani kuokoa data zinazopotea kwa bahati mbaya kwenye vifaa vyako vya elektroniki?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com