Misheni ya Juno : Mambo yote ya kuyajua kuhusu Safari hii ya NASA - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Misheni ya Juno : Mambo yote ya kuyajua kuhusu Safari hii ya NASA

1
Sambaza

where can i buy priligy in uk Baada ya safari ya miaka Mitano angani, leo chombo cha anga cha Marekani, Juno kumeifikia sayari ya Jupita katika Misheni ya kihistoria tangu utafiti wa anga kuanza kufanyika.

http://myownclarity.com/2017/02/

follow site Haya ni mambo ambayo yatakupa mwanga kuhusu safari hii;

PIA13746-16

Safari hii inahusiana na nini?

Wanasayansi wanajaribu kufumbua fumbo la nini kinapatikana chini ya wingu zito ndani ya sayari ya Jupita. Machache sana yanajulikana kuhusiana na gesi nzito iliyotanda kuizunguka sayari hii ambayo huonekana kupitia Darubini za masafa ya mbali.

Kwa nini Misheni ya Juno imetiliwa Mkazo zaidi?

Chombo hiki, ambacho kimepewa jina mungu wa Kiroma, Jupiter na mkewe imefungashiwa vifaa nane muhimu ambayo vitakiwezesha chombo hiki kuingia mpaka katika kitovu cha sayari ya Jupiter bila matatizo. Hivyo ni matumaini ya wanasayasi wengi kuwa, misheni hii itavumbua mengi zaidi kuhusiana na Sayari hii. Pia chombo hiki kimeruka Maili 2,600 karibu zaidi kuliko chombo kingine chochote katika anga za juu.

INAYOHUSIANA  Ijue ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner

Inawezekana mambo kwenda Kombo?

Mwanzo kilichohofiwa zaidi ni wakati wa chombo hiki kuingia katika njia ya Sayari hii (Orbit System) kwani ni Sayari inayozunguka kwa kasi sana na kurusha uchafu mwingi, ikiwa ni pamoja na majabali makubwa sana.

05_solar_lb

Sayari hii inazunguka kwa kasi sana na kurusha uchafu mwingi, ikiwa ni pamoja na majabali makubwa sana.

“Tunachofanya ni kwenda Karibu zaidi, kukusanya data na kuondoka. Kuingia kwa mara ya kwanza katika sayari kama hii, hiyo ndio hatari kubwa zaidi. Anaelezea mwanasayansi mkuu wa Juno, Scott Bolton kuhusu Jupiter.

Nini kitatokea Juno ikifika katika Sayari ya Jupiter?

Juno ni chombo cha kwanza cha anga kufikia kwa ukaribu zaidi sayari hii. Hii ni kutokana na umbali wa sayari hii kutoka katika Jua na nguvu za Nyuklia.

Pamoja na kuchukua safu ya vipimo kisayansi, kamera zilizofungwa katika chombo hiki zitatumia Mwaka Mzima kupiga picha kwa ukaribu zaidi kuliko misheni yeyote ile.

INAYOHUSIANA  NASA, Uber kuleta usafiri wa anga katika miji yenye watu wengi

Hii itasaidia wanasayansi kuelewa Doti kubwa Jekundu katika sayari hii linahusu nini –  na dhoruba lenye umbo la jicho- linaloizunguka sayari hii na kupungua

Je, chombo hiki kitarudi duniani ?

Hapana.

juno20120830-640

Juno kimechukua miaka 5 angani kabla ya kufikia Sayari hii

Mara baada ya kazi hii Jupita, chombo hiki cha Juno kitajitupia katika vumbi zito la Jupita na kuungua angani. Hii yote ni  kuepuka ajali za chombo kuanguka katika moja ya sayari zinazozunguka Mwezi.

Sayari ya Jupiter inadhaniwa na wanasayansi kuwa sayari ya kwanza kabisa kuundwa katika mfumo wa jua na ilionekana kwa mara ya kwanza na Wababiloni wa karne ya 8KK

Kwa ufupi kabisa, Misheni ya Juno ina mambo yafuatayo muhimu kuyajua!

  1. Chombo cha NASA cha Juno  kitakuwa chombo anga cha kwanza kupita chini ya wingu nene la Jupiter
  2. Juno kilianza safari mnamo Agosti , 2011, na imekuwa ikisafiri angani kwa miaka mitano mfululizo.
  3. Tangu kuruka kwake kutoka duniani mpaka katika njia ya Jupita, Juno kimesafiri kilomita milioni 2,800 ambazo ni zaidi ya mara 18 ya wastani wa umbali kutoka duniani na Juani.
  4. Ni safari ya mara ya kwanza ya chombo kuendesha kwa kutumia nishati ya jua kutoka Duniani.
  5. NASA walikua na Nafasi MOJA tu kufikisha chombo hiki Jupita, kwamba wakishindwa hiyo basi isinge wezekana tena kuingia obiti ya Jupiter .
  6. 118728-large_trans++qVzuuqpFlyLIwiB6NTmJwfSVWeZ_vEN7c6bHu2jJnT8 Wakati Juno inapokaribia Jupiter, mvutano wa sayari hii kuvuta chombo hiki ulikua wa kasi ya ajabu, na kusababisha, ili kwenda sawa na kasi ya mzunguko wa sayari hii, chombo hiki kwenda kasi ya kilomita zaidi ya 250,000 kwa saa za dunia. Hii inafanya chombo hiki kuwa chombo pekee duniani chenye kasi hii kuwahi kutengenezwa na mwanadamu.
  7. Safari hii imegharimu jumla ya dola bilioni 1.13   na ‘project’ nzima itakamilika baada ya miaka miwili.
INAYOHUSIANA  Uhai wa tafiti za kisayansi nchini Uingereza

Inategemea kufikia Februari mwaka 2018 kifaa hicho kitadondoka na kuungua katika anga la sayari hiyo. Na baada ya hapa kazi ya kusoma data/taarifa zote zilizotumwa duniani inaweza chukua muda wa ata miaka miwili zaidi.

Vyanzo : The Telegraph, BBC, NASA na YKE

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author