Misheni ya Juno: Picha ya kwanza ya Jupiter yatolewa - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Misheni ya Juno: Picha ya kwanza ya Jupiter yatolewa

0
Sambaza

Chombo cha anga za juu cha shirika la Marekani la NASA kilichopewa jina Juno kimetuma picha yake ya kwanza ya sayari ya Jupiter.

Mission+to+Jupiter

here Moja ya picha hizo iliyotolewa na NASA Jumanne inaonesha sayari hiyo ikiwa imezungukwa na miezi mitatu kati ya miezi yake minne mikubwa.

http://bountifulplantsblog.com/about-2/ Soma Pia – Misheni ya Juno : Mambo yote ya kuyajua kuhusu Safari hii ya NASA

picha ya kwanza ya Jupiter

go here Picha ya kwanza ya sayari ya Jupiter

Miezi inayoonekana ni Lo, Europa na Ganymede. Mwezi huo mwingine uitwao Callisto hauonekani. Picha hiyo ilipigwa Jumamosi sayari Juno ilipokuwa inazunguka sayari hiyo ikiwa umbali wa maili milioni tatu.

Hata katika umbali huo Shimo Jekundu lililosababishwa na dhoruba kali kwenye sayari hiyo karne nyingi zilizopita, linaonekana. Juno iliingia katika mzingo wa Jupiter wiki iliyopita na kuanza kuizunguka sayari hiyo ambalo pia hufahamika kama Zohali au Zozali.

INAYOHUSIANA  NASA, Uber kuleta usafiri wa anga katika miji yenye watu wengi

Safari yake kutoka duniani hadi ilichukua miaka mitano. Juno itachunguza na kupeleleza sayari hiyo kwa miezi 20, lengo kuu likiwa kusaidia wanasayansi kubaini asili ya sayari hiyo ambayo wanaamini inaweza kuwasaidia kuelewa zaidi asili ya mfumo wa Jua.

Chombo hicho cha juu kilipokuwa kinaikaribia Jupiter, kamera zake na mitambo mingine muhimu vilizimwa kuzuia visiharibiwe na miali nururishi na baadaye vilifunguliwa. Picha hiyo ni muhimu kwa sababu inaonyesha kuwa Juno imefanikiwa kufika.

Wanasayansi wanatarajia picha za karibu zaidi za Jupiter zitapokelewa mwezi ujao na NASA inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018.

Baadhi ya Wanasayansi walioko katika sayari ya Jupita

Baadhi ya Wanasayansi walioko katika timu ya inayowezesha safari ya Juno

Baadhi ya sifa za Sayari ya Jupita

  •  Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na
  • uzito wake ni mara 300 zaidi.
  • Sayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja huko hudumu saa 10.
  • Muundo wake ni kama wa nyota
  • Kuna gesi ya Haidrojeni na Helium.
INAYOHUSIANA  Ijue ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner

Soma Pia – Misheni ya Juno : Mambo yote ya kuyajua kuhusu Safari hii ya NASA

Kufanikiwa kwa Juno katika safari ya kufika katika sayari ya Jupita kunaiongezea heshima NASA na hamasa kwa mashirika mengine ya anga kuweza kufanya kitu kama hicho au zaidi ya hicho.

Vyanzo: BBC, Independent

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.