Magwiji ya mitandao ya kijamii yaungana dhidi ya meseji za kigaidi

0
Sambaza

Magwiji wa mitandao ya kijamii kama Facebook, Microsoft, Youtube na Twitter wamekubaliana kuunda kundi la kikazi la kimataifa litakalokuwa likishughulika kuondoa ujumbe au maudhui yoyote yanayoashiria kazi za kigaidi mitandaoni.

Hatua hiyo ya kampuni hizo za mitandao ya kijamii imefanyika kufuatia shinikizo hasa kutoka Marekani na Ulaya kwa kuwataka kuwa na ufumbuzi wa kuondoa ujumbe wowote unaoonekana wenye maudhui ya kigaidi.

meseji za kigaidi

Ujerumani wameunda sheria itakayo toa faini ya uero milioni 50 kwa mtandao wowote wa kijamii ambao utashindwa kufuta ujumbe wa kigaidi uliowekwa katika mtandao husika.

SOMA PIA:  Saudi Arabia yaondosha marufuku ya kupiga simu za Skype, WhatsApp na Viber

Makampuni hayo yameahidi kuanzisha suluhisho la kiteknolojia la pamoja kupiga vita ugaidi mitandaoni.

Je wewe una mtazamo gani juu ya utumiaji mbovu wa mitandao ya kijamii unaoweza kuleta madhara kwa jamii na ulimwengu kwa ujumla?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com