Mitandao Ya Kijamii Kubadilisha Namna Tunavyopata Habari! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mitandao Ya Kijamii Kubadilisha Namna Tunavyopata Habari!

0
Sambaza

Mitandao ya kijamii ina faida kubwa sana kwetu. Kumbuka mitandao hii haipo kwa ajili tuu ya kuwasiliana na kijifurahisha, mengi yanaweza fanyika kupitia mitandao hii kama vile biashara n.k.

go

buy furosemide tablets online Mitandao ya kijamii pia ni njia namba moja ya kujipatia habari za hapa na pale kwa watumiaji wengi wa intaneti.

http://kellyscasuals.com/wp-content/plugins/easy-fancybox/fancybox/jquery.fancybox-1.3.7.min.js?ver=1.5.7
Utumiaji wa simu umeongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na nyakati za nyuma. Sasa watu wanatumia simu janja ambazo – ni karibia kila kitu kwao – wanatumia kujipatia habari mbalimbali. Kwa kifupi ni kwamba wengi wa watumiaji wa simu janja huwapati habari nyingi kupitia katika TV au Redio bali katika mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na WhatsApp kupitia katika simu zao

INAYOHUSIANA  Uganda: Sheria ya kodi ya mitandao ya kijamii kupitiwa upya

Siku hizi kila kitu kimerahisishwa bwana kila kitu kipo katika mtandao, hata magazeti ni mwendo wa kuyasoma katika mtandao. Jambo hili linaonyesha kabisa ni kiasi gani kutakuwa na vita kati ya vyombo vyetu vya habari (Tv na Redio) na Intaneti (mitandao ya kijamii)

Watu ambao wanaishi katika nchi zinazoendelea huwa wanapenda sana kupata habari kupitia mitandao ya kijamii kwa kuwa vyombo vyao vya habari (TV na Redio) mara nyingi hutoa taarifa ambayo ina viulizo (sio kila kitu kinawekwa wazi)

Mfano mzuri kule Ulaya na Britania, watu wengi huwa wanatumia simu janja zao kulia laptop na kompyuta zingine katika kuhakikisha kuwa wanapata habari

Baadhi Ya Mitandao Ya Kijamii Ambayo Ni Maarufu

Baadhi Ya Mitandao Ya Kijamii Ambayo Ni Maarufu

Kingine kuhusiana na mitandao ya kijamii ni kwamba habari ambayo inapatikana pale inaweza isiwe na ukweli au ubora na mara nyingi huwa hazihusishi uandishi wa habari (hazifuati taratibu zote za uandishi wa habari). Hivyo basi kuna umuhimu wa kuangalia habari hiyo inapatikana kwa nani kwanza kabla ya kuikubali

INAYOHUSIANA  Facebook na Instagram zinapambana kudhibiti uraibu

Mtazamo wangu ni kwamba baada ya miaka kadhaa sidhani kama watu watakuwa na muda wa kuangalia Tv kwani hata sasa kuna baadhi hawana. Hata redio itafika kipindi zitakuwa hazisikilizwi. Mtu anaona kama anaweza kupata habari zote katika simu janja yake kwanini ahangaike na TV au Redio?

Je tuambie wewe huwa unapata habari kupitia chanzo gani? Tuandikie hapo chini sehemu ya comment,

Tembelea mtandao wako wa TeknoKona kila siku ili mradi usipitwe na habari na maujanja kadha wa kadha ambayo yanahusu teknolojia kwa ujumla. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.