fbpx

Mkebe wa kuhifadhi AirPods kuwa na uwezo wa kuchaji iPhone

1
Sambaza

Moja kati ya bidhaa zinazofanya vizuri sokoni kutoka kwa kampuni nguli ni AirPods ambazo zinaonekana kusambaa (kununuliwa) hivyo watu wengi kuwa nazo lakini pengine wateja wa Apple na ulimwengu kwa ujumla wakafurahi zaidi!.

Naamini utakuwa unafahamu vyema ule mkebe wa kutunza zile AirPods ambazo zinavutia kweli kweli hasa kwa jinsi zilivyoundwa na kutoona hata chembe ya waya isipokuwa zenyewe tu ambazo ni ndogo na kamwe hazichoshi kuwa nazo popote pale.

Kwa taarifa zilzosambaa kwenye tovuti mbalimbali inaaminika kuwa Apple wapo kwenye mpango wa kuwezesha mikebe ya kutunza AirPods kuwa na uwezo wa kuchaji iPhone 8, 8+ au X.

Mkebe wa kuhifadhi AirPods

Mikebe hiyo kuwa na uwezo wa kuchaji simu ni kitu ambacho watu wengi walikuwa wakisubiri.

Teknolojia inayozungumziwa hapa na kuwa uti wa mgongo katika kufanikisha suala hilo ni kuchaji simu janja bila kutumia chaji ya waya nikiwa na maana kuchaji simu kwa teknolojia ya bila waya ambapo iPhone 8 na kuendelea ina uwezo huo.

Visit Your URL Teknolojia hii huenda ikaanza kuonekana kwenye mikebe ijayo ya AirPods itakayotolewa mwezi Septemba kama ilivyo desturi ya Apple kutoa simu mpya (iPhone) pamoja na bidhaa nyingine mwezi huo.

Teknolojia ya kuchaji AirPods ambapo iwapo mkwbw wake unakuwa na umeme basi spika hizo za masikioni ziapata chai bila ya kutumia waya.

Hakuna uhakika sana kuhusu mikebe hiyo ya kuhifadhia kutoka mwezi Septemba 2018 lakini inaaminika kuwa iwapo teknolojia hiyo ikiongezwa itawasaidia Apple kuuza AirPods zaidi ya 28 milioni.

Vyanzo: Engadget, 9to5mac

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Punguzo la bei ya betri kwa simu za iPhone
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|