Mkongo wa intaneti wa Taifa wajengwa kwa kilomita 26,961 - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mkongo wa intaneti wa Taifa wajengwa kwa kilomita 26,961

0
Sambaza

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amesema Serikali mpaka sasa imejenga kilomita 7,560 za mkongo wa Intaneti wa Taifa kutokana na mkopo nafuu iliyoupata kutoka nchini China.

buy Finax online hong kong Aidha, ameongeza kuwa sekta binafsi kupitia umoja wa kampuni za simu imejenga kilomita 1,401.26. Vilevile, kampuni ya Halotel nayo imejenga kilomita 18,000 na hivyo kufanya jumla ya kilomita 26,961.26 za mkongo wa taifa kujengwa nchini.

source Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye

Mkongo wa Taifa umefika kwenye mikoa yote na mipakani mwa nchi za jirani zisizopakana na bahari za Uganda, Rwanda, Zambia, Burundi na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

> Ushirikiano na Viettel/Halotel

Serikali ina makubaliano na kampuni ya Viettel inayomiliki Halotel, kufikisha huduma ya mawasiliano kwenye vijiji 4,000 na tayari, mpaka Februari, walikuwa wameviunganisha vijiji 3,712 na ujenzi unaendelea kwa vijiji 288 vilivyosalia mwaka 2018/19.

INAYOHUSIANA  Smile Telecom ya Uganda yawalipia wateja wake kodi ya mitandao kwa miezi mitatu

> Watumiaji wa intaneti Tanzania

Kutokana na maeneo mengi nchini kuunganishwa kwenye mkongo huo, taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha matumizi ya intaneti yameongezeka kutoka zaidi ya watumiaji milioni 19.86 waliokuwapo Desemba 2016 hadi milioni 23 Desemba mwaka jana.

Naibu waziri anasema hadi mwaka 2020, matumizi ya intaneti yataongezeka zaidi kutokana na kushamiri kwa mifumo ya kieletroniki katika sekta zote kama vile ukusanyaji wa malipo kwa njia ya mtandao, matokeo ya mitihani, usajili wa vyuo vikuu na vya ufundi, afya na elimu mtandao, usajili wa vizazi na vifo (Rita) na Usajili wa Biashara (Brela).

Mawasiliano vijijini Wakati matumizi ya simu za mkononi kufanikisha huduma za fedha zikiipa Tanzania sifa nje ya mipaka yake, yapo baadhi ya maeneo hayana mtandao huo wa mawasiliano.

INAYOHUSIANA  Downloading vs Streaming : Fahamu Tofauti Kuu, Kipi bora zaidi?

Hata hivyo, hali inaendelea kuwa nzuri kwani asilimia 94 ya wananchi wote nchini wanapata huduma za mawasiliano na Serikali imetoa ruzuku kwa kampuni za simu nchini kujenga minara na kufikisha huduma hizo maeneo ambayo hayajaunganishwa.

http://greatstridesofneiowa.org/?feed=comments-rss2 “Hadi sasa, Serikali imetoa Sh95 bilioni kufikisha mawasiliano vijijini na tayari kata 451 zimepata mawasiliano kupitia ruzuku ya Serikali,” anasema Nditiye. Anafafanua kuwa, katika mwaka wa fedha wa 2017/18, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umetoa zabuni ya kufikisha huduma ya mawasiliano katika kata 75 zenye vijiji 154, ambapo kata nane zenye vijiji 15 zimekamilika na mpaka Juni, 67 zilizobaki zitakuwa zimekamilika pia.

Miongoni mwa maeneo yaliyopewa kipaumbele ni kuendeleza ujenzi wa mkongo wa Taifa kwa dhamira ya kufikisha huduma zake makao makuu ya wilaya zote nchini.

INAYOHUSIANA  Intagram yaenda mbali, sasa inawatumiaji hai bilioni moja

Wakati wilaya zote zikitarajiwa kuunganishwa kwenye mkongo huo, mkakati wa kusimamia na kudhibiti mapato ya Serikali unao umepewa kipaumbele. Kufanikisha hilo, Serikali inaratibu ujenzi wa vituo vya kutunza data, Dodoma na Zanzibar.

Pamoja na mafanikio yaliyobainishwa, juhudi bado zinatekelezwa kuhakikisha sekta ya mawasiliano inaongeza tija kwa Taifa na maisha ya wanananchi kwa ujumla.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.