Mkurugenzi wa Apple ameanza kutumia iPhone 8 ambayo haijazinduliwa rasmi?

0
Sambaza

Picha ya Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Apple bwana Tim cook aliyopigwa akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa CTS huko Cincinnati, Ohio nchini Marekani, inaonesha mfuko wa suruali yake ukiwa umetuna kwa kubeba simu inayodaiwa ni iPhone 8.

Uvumi huo unatoka kwa mashabiki walioonesha hisia zao kwamba simu iliyo mfukoni mwa Tim Cook ni iPhone 8 kutokana na urefu ulijitokeza kwenye mfuko wa suruali yake.

Mkurugenzi wa Apple ameanza kutumia iPhone 8

Mkurugenzi wa Apple ameanza kutumia iPhone 8?

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Apple waliwahi kueleza kwamba Iphone 8 itakuwa ndefu kuliko Iphone 7 Plus.

SOMA PIA:  Apple yafanya masasisho kwenye iOS 11.1 kurekebisha mambo mbalimbali

Tim Cook alitoa picha hiyo katika akaunti yake ya Twitter akiwashukuru wafanyakazi wa CTS kwa ufanisi mzuri wa majaribio ya vifaa vya kampuni ya Apple.

Hata hivyo wengine walionesha utani kwamba Mkurugenzi huyo anatumia Samsung Galaxy 8 kitu ambacho si kweli.

Wafatiliaji wengi wa Simu Janja wamekuwa na hamu kubwa ya kuijua na kuiona simu mpya ya Iphone 8 ambayo inatarajiwa kuinduliwa hivi karibu.

Joto la uzinduzi wa simu hiyo limekuwa likipanda kwani ni mara kadhaa umeahirishwa na kutowekwa sababu za wazi, kiasi cha kuwa na tetesi simu hiyo imekuwa na matatizo kadhaa yanayopelekea kuahirishwa uzinduzi wake.

SOMA PIA:  AzamTV App yapakuliwa zaidi ya mara milioni moja

Msomaji wetu waonaje je ni kweli unadhani ni Iphone 8 ndio iliyokuwa ndani ya mfuko wa suruali yake? Tupe maoni yako.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com