Mkutano wa pili wa Africa Open Data waanza nchini Ghana - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mkutano wa pili wa Africa Open Data waanza nchini Ghana

0
Sambaza

Mkutano mkubwa wa pili wa Africa open Data Conference (AODC) umeanza Julai 17 nchini Ghana katika ukumbi wa kimataifa wa Accra International Conference Centre.

Mkutano huo unafanyika kwa siku nne kuanzia Julai 17 mpaka Julai 21.

Mkutano wa kwanza ulifanyika Septemba 2015 nchini Tanzania ulioandaliwa na Serikali ukiungwa mkono na World Bank, Code for Africa, Global Open Data for Agriculture & Nutrition initiative, Worldwide Web Foundation, MCC, na wadau wengine.

http://lbsprouting.com/\

Mkutano huo wa siku nne utahusisha mafunzo ya vitendo kwa wajasiriamali, mabalozi na wafanyakazi wa kuhifadhi data mbalimbali.
Mkutano huo umevutia watu wengi ambapo wajumbe 600 kutoka nchi za Afrika nzima na duniani kote wamehudhuria.

Phenytoin buy fast Mahadia Tunga

Mkutano huo unatarajiwa kusukuma viongozi wa kiserikali na sekta binafsi katika kusambaza, kutumia na kudai uwazi katika taarifa zao. Pia mkutano huu utasaidia kuwaweka pamoja wafadhili, wawekezaji watakaosaidia kupanua na kuharakisha maendeleo katika nchi za Afrika na dunia kwa ujumla.
Aidha, Kuendeleza na kupanua ushirikiano ambao hujenga ufahamu wa data wazi na kuendesha matumizi ya data wazi katika ya biashara, vyombo vya habari, serikali, wasomi, mashirika ya kiraia, wananchi, na mashirika ya utetezi.

Katika mkutano huo Tanzania inawakilishwa na mkuu wa mafunzo ya uhifadhi wa data (Tanzania Data Lab: dLab), katika chuo kikuu cha Dar es salaam, Mahadia Ali Tunga.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Fahamu mfumo mpya usajili wa laini za simu
Share.

About Author

can you buy antabuse over the counter Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.