fbpx

Mlipuko wa simu waripotiwa kumuua Mkurugenzi Mtendaji wa Malaysia

0
Sambaza

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Fedha la mradi wa Cradle Fund la Malaysia, Nazrin Hassan ameripotiwa kufa kutokana na majeraha aliyoyapata yaliyosababishwa na mlipuko wa simu ya mkononi.

buy Lyrica in australia

Awali ilielezwa sababu ya kifo chake ni tatizo la kupumua lakini kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Cradle, Nazrin Hassan alikufa kwa matatizo ya majeraha aliyoyapata kichwani kutokana na mlipuko wa simu wakati alipokuwa amelala.

Haijajulikana ni simu aina gani iliyolipuka na kusababisha kifo chake. Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Malaysia kutoka kwa familia ya Hasssan zinaeleza alikuwa na simu mbili moja BlackBerry na nyingine Huawei, lakini haijafamika ni ipi iliyolipuka.

Mlipuko wa simu

Marehemu Nazrin Hassan alikufa kwa matatizo ya majeraha aliyoyapata kichwani kutokana na mlipuko wa simu wakati alipokuwa amelala.

Matukio ya kulipuka kwa simu na kusababisha vifo kwa watu yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara hususani pale ambapo utaratibu mzuri wa matumizi yake unapokiukwa mathalani kuchaji simu na kuitumia kwa wakati huo huo.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Xiaomi yafungua zaidi ya maduka 500 kwa wakati mmoja
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.