Jeffrey Bezos, Mmiliki wa Amazon ampiku Bill Gates kwa utajiri duniani

Jeffrey Bezos: Mmiliki wa Amazon ampiku Bill Gates kwa utajiri duniani

0
Sambaza

Jarida la Forbes, limetoa orodha ya matajiri wa kupindukia duniani na kumtaja mmiliki wa Kampuni ya Amazon, Jeffrey Preston Bezos kuwa kinara katika orodha hiyo.

order celexa Utajiri wa Bezos umepanda na kufikia dola bilioni 112 kutoka takriban dola bilioni 39.2 za mwaka jana. Jeffrey Bezos ndiye mmiliki na mwanzilishi wa Mtandao maarufu  duniani wa uuzaji na ununuzi bidhaa mbalimbali.

Gates ameongoza orodha hiyo kwa miaka 18 kati ya miaka 24 iliyopita.

Jeffrey Bezos

Jeffrey Bezos, mmiliki wa Mtandao wa Amazon

Miongoni mwao, kuna mabilionea 259 wapya ambao walijipatia utajiri wao kutoka katika biashara za aina nyingi zikiwemo nguo za harusi, wanasesere wa kuchezewa na watoto na magari yanayotumia umeme.

INAYOHUSIANA  Apple na Oprah kufanya kazi kwa pamoja

Marekani ndiyo nchi inayodaiwa kuwa na mabilionea wengi duniani, ambapo ina mabilionea 585, ikifuatwa na China. Jimbo la California pekee lina mabilionea 144, zaidi kushinda mataifa yote isipokuwa Marekani na China.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.