fbpx

Mobile Airbag: Kifaa Cha Kuzuia Simu Kupasuka

0
Sambaza

Tatizo la vioo vya simu kupasuka katika simu janja nyingi limekua kila siku likitafutiwa  utatuzi lakini bado hali hiyo imezidi kutokea pengine kutokana na njia za kuzuia jambo hilo bado imekua ikipata changamoto kubwa.

buy isotretinoin now

Kutana na kijana wa miaka 25 kutoka Ujerumani, Philip Frenzel mwanafunzi wa chuo ambae ametengeneza kifaa maalum ambacho kinasaidia simu kutokupata hitilafu yoyote pindi inapoanguka.

Mobile Airbag inafanyaje kazi?

Kifaa hicho unakivalisha katika simu yako mfano kama wa kasha la simu ambapo pindi simu itapokua inaanguka kifaa hicho kimewekewa teknolojia maalum ambayo itahisi na kisha kutoka katika pembe nne za simu hiyo zitajifungua na kutokea kama miguu minne ambayo ina vitu maalum ambazo vitafanya simu iweze kunesa tu bila kupata madhara yoyote.

Kupasuka

Teknolojia hii mpya imeonekana kuwa tofauti na zingine ambazo nazo husaidia simu kutokupata madhara pindi inapoanguka, ambapo hii inafanya kifaa chako kiwe salama kwa kuhakikisha simu haigusi ardhi.

Mpaka sasa bado Mobile Airbag inaendelea kufanyiwa majaribio ili kuweza kuboreshwa zaidi ambapo inatazamiwa kuanzia mwezi huu (Julai) huenda kifaa hicho kikaanza kuuzwa sehemu mbalimbali.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Samsung Galaxy yenye 5G haipo mbali
Share.

About Author

Mwandishi Pia mpenzi mkubwa wa masuala ya Teknolojia, Napenda Kujifunza, Karibu Tujifunze Pamoja.

Comments are closed.