Wiki hii imekuwa ni simu baada ya simu kwenye maonyesho ya IFA 2018 huko Berlin-Ujerumani na moja ya rununu iliyoletwa machoni pa watu ni Motorola One na One Power.
Makampuni mbalimbali yamekuwa yakitumia mkutano huo kutoa simu janja ambazo safari hii angalau kwa simu ambazo tumeshazizungumzia bei zake ni stahimilivu (sio ghali) zikiwemo Motorola One/One Power ambazo zimetoka kwa pamoja.
Katika mchanua wa leo nimeamua nichambue simu hizi katika namna rahisi na nyepsi ambayo itakuwa ni rahisi kueleweka:
Kipengele |
Motorola One |
Motorola One Power |
RAM | GB 4 | GB 4 |
Mega Pixels (MP) | Kamera ya Mbele: 8MP na Kamera za Nyuma: Zipo 2; MP 13+2MP | Kamera ya Mbele: 12MP+LED flash na Kamera za Nyuma: Zipo 2; MP 16+5MP pamoja na LED flash 2 |
Picha jongefu | Ina uwezo wa kurekodi picha mnato zenye ubora wa 4K. | Ina uwezo wa kurekodi picha mnato zenye ubora wa 4K. |
Uwezo wa Betri | 3000mAh, halitoki pia linakaa na chaji kwa siku nzima pia ina teknolojia ya kuchaji haraka; inachukua dakika 20 tu kujaa chaji. | 5000mAh, halitoki pia linadumu na chaji kwa muda wa siku mbili (kwa matumizi yoyote). Vilevile, ile teknolojia ya kuchaji simu haraka inachukua robo saa kulifanya betri liwe limejaa. |
Kipuri mama | Qualcomm Snapdrago 625, kasi yake ni 2 GHz | Qualcomm Snapdrago 636, kasi yake ni 1.8 GHz |
Mawasiliano | GSM / HSPA / LTE | GSM / HSPA / LTE |
Memori ya Ndani | GB 64 | GB 64 |
Memori Kadi? | Inaruhusu kuongeza mpaka GB 256 | Inaruhusu kuongeza mpaka GB 256 |
Uwiano wa kioo | 19:9 | 19:9 |
Aina Ya Kioo | IPS (LCD) | IPS (LCD) |
Ukubwa Wa Kioo | Inchi 5.9 | Inchi 6.2 |
Utambuzi Wa Alama Za Vidole? | Ndio – Upo Kwa Nyuma | Ndio – Upo Kwa Nyuma |
Rangi | Nyeusi | |
Ukubwa (Wembamba) | 150 x 72.2 x 8.0mm | Sm 17.5 |
Muonekano | Umbo lake linatengenezwa na kioo (Gorilla 2.5 pande wa nyuma na mbele) pamoja na chuma. Kuna sehemu ya kuchomekaspika za masikioni. | Umbo lake linatengenezwa na kioo (Gorilla 2.5 pande wa nyuma na mbele) pamoja na chuma. Kuna sehemu ya kuchomekaspika za masikioni. |
Simu zote mbili zinatumia Android 8.1 Oreo (Android One), simu zote zitapokea masasisho ya kuhamia kwenye Android 9 Pie katika siku za usoni na Google wameahidi kutoa masasisho ya kuzilinda simu hizo katika kupindi cha miaka mitatu.
Motorola One inauzwa kwa karibu $347|Tsh. 798,100 na Motorola One Power bei yake bado haijatangazwa ikitazamiwa kuanza kupatikana duniani kote kuanzia mwezi Oktoba.
Vyanzo: CNET, The Verge, Engadget, XDA
One Comment
Comments are closed.