Move to Android: Apple Kutengeneza App ya Kusaidia Watumiaji wake Kuhamia Simu za Android - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Move to Android: Apple Kutengeneza App ya Kusaidia Watumiaji wake Kuhamia Simu za Android

0
Sambaza

Baada ya kubanwa na kupewa lawama sana na mashirika ya simu kutoka bala la Ulaya inaonekana kuna uwezekano mkubwa ya kwamba kampuni ya Apple ipo katika utengenezaji wa app itakayowasaidia watumiaji wake kuhamisha data zao kwa urahisi kwenda kwenye simu za Android.

simu-iphone-android

Habari hii imevujishwa kupitia mtandao maarufu wa habari wa Telegraph huku wakidai chanzo kikuu ni mtu wa ndani kutoka moja ya makampuni makubwa ya simu ya balani ulaya.

Je ni nini kitakuwa rahisi kuhamishika kama hili jambo ni la kweli?

Kwa muda mrefu Tume inayohusika na masuala ya biashara balani Ulaya pamoja na makampuni ya simu yamekuwa yakiibana Apple kufanya iwe rahisi watumiaji wa simu hizi kuamisha data kama vile picha, video na muziki kwenda kwenye simu za Android.

INAYOHUSIANA  Motorola inatarajiwa kutoa simu janja

Makampuni ya simu yamekuwa yakidai kampuni ya Apple inatengeneza mazingira magumu kwa watumiaji wa simu hizo kuhama kwani imekuwa ni vigumu wao kuhamisha data zao muhimu kwa urahisi.

Move to Android: Tayari kuna app kutoka Apple inayoitwa Move to iOS inayowasaidia watumiaji wa Android kuhamisha data zao kwa urahisi kwenda kwenye simu ya iOS na wadau wanadai Apple naye afungue milango kwenye iOS kufanya iwe rahisi watumiaji wake kuhamisha data kwenda simu za Android.

android-move-to-ios

Muda utaleta majibu ya uhakika!

Kwa sasa ni vigumu kufikiria uamuzi huo, ila kutokana na msukumo wa muda mrefu kutoka balani Ulaya ni jambo ambalo linaweza kufanywa na Apple ila kuhakikisha kampuni hiyo inaendelea kuwa na mahusiano mazuri na makampuni na vyombo vya sheria vya nchini humo.

INAYOHUSIANA  iPhone X yadumu kwa wiki mbili chini ya mto

Mwandishi Christoper Williams wa mtandao wa Telegraph hakupata majibu kutoka Apple pale alipojaribu kuulizia juu ya taarifa hizi.

Je una maoni gani? Unafikiri ni jambo zuri kwa Apple kulifanya? Na je unafikiri ni jambo wanaloweza fanya?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply