fbpx

Msichana anusurika kifo kwa sababu ya ‘Selfie’

0
Sambaza

Msichana (Jina limehifadhiwa) wa Urusi katika jiji la Moscow mwenye umri wa miaka 13 amenusurika kifo alipoangukia waya za umeme kutoka kwenye daraja la reli wakati alipokuwa akijipiga selfie.

Picha zilizochapishwa na mashirika ya habari zilionyesha msichana huyo akining’inia kwenye waya za umeme.

Maafisa wa serikali walinukuliwa kusema kwamba msichana huyo alikuwa akirudi nyumbani na marafiki wake ndipo http://skunkslist.com/?feed=rss2 alipoamua kwenda pembeni mwa daraja kujipiga selfie wakati treni ya kusafirisha mizigo ilipokuwa ikikaribia, lakini kwa bahati mbaya akaanguka.

Wasamaria wema walimkimbiza hospitalini kwani alikuwa ameungua katika sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mkononi, mabegani na mguu wa kushoto.

kifo

Inaelezwa alining’inia hapo kwa takribani saa moja kabla kuonekana na mwendesha gari moshi ambaye aliwapigia simu wasimamizi wa usambazaji umeme katika shirika hilo la treni wazime umeme uliokuwa ukipitishwa kwa nyaya hizo.

Kulingana na ripoti za habari, mpita njia alitumia kamba kumvuta kumrudisha darajani huku wanakijiji wengine wakishikilia zulia kubwa chini yake endapo angeanguka.

INAYOHUSIANA  Simu za makampuni ya China zashika robo ya soko la simu Ulaya

Madaktari walinukuliwa wakisema alipata pia jeraha kichwani na alipopata fahamu baadae hakuweza kukumbuka kilichotokea. Tahadhari! Ni muhimu kuangalia maeneo ya kuchukulia selfie vinginevyo unaweza kuchungulia kifo.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.