Mtandao gani wa simu ni nafuu zaidi? Upi unakua kwa kasi? – Data za TCRA

0
Sambaza

Ripoti ya robo ya pili ya mwaka huu iliyotolewa na TCRA inatoa picha nzuri juu ya gharama na ukuaji wa huduma za mitandao ya simu. Ripoti hiyo ya mwisho wa mwezi wa sita mwaka huu inakupa picha ya mtandao gani wa simu ni nafuu zaidi, na pia ukuaji wa mitandao hiyo.

Tuanze na ukuaji;

Mtandao wa Halotel na Airtel ndio wamekuwa kwa kasi zaidi katika miezi ya tano na sita mwaka huu kuliko mtandao mwingine wowote wa simu. Wakati Halotel walipata wateja wapya 218,588, Airtel walipata wateja 136,862, wakati Tigo walipata wateja 113,703 na huku Vodacom wakipoteza wateja 5,673 (yaani hawakuwa na ukuaji kabisa).

SOMA PIA:  BRELA: Usajili wa Kampuni na Biashara sasa kwa Mtandao

Data za ukuaji wa wateja wapya.

Data zinazoonesha ukuaji kwa miezi ya tano na sita mwaka huu

Je mtandao gani ni nafuu zaidi?

  • Gharama za maongezi – simu za maongezi
mtandao gani wa simu ni nafuu zaidi

Wastani wa gharama za maongezi katika Tsh kwa kila dakika ya maongezi kwa simu za wateja wa mtandao huo huo – (bila kujiunga vifurushi)

Gharama kwa simu za kwenda mitandao mingine (mfano: mtu wa Airtel akipiga kwenda mitandao mingine). Bei ni kwa dakika (Tsh)

Gharama za SMS (UJumbe mfupi)

  • SMS za ndani ya nchi
Gharama za ujumbe mfupi

Gharama za ujumbe mfupi (SMS) kwenda mitandao mbalimbali (nje ya kifurushi)

  • SMS kwenda nje ya nchi
Gharama za ujumbe mfupi

Gharama za ujumbe mfupi kwenda nje ya nchi

Soko la huduma za kibenki za mitandao ya simu kufikia Juni 2017;

Ukuaji wa huduma za kibenki za simu

Ukuaji wa huduma za kibenki za simu, Airtel Money imeendelea kukua na sasa inashindana moja kwa moja na Tigo Pesa kwenye idadi ya watumiaji

Kwa ufupi;

  • Mtandao wa Tigo ingawa ni maarufu sana umekuwa ni mmoja wa mtandao wenye gharama za juu sana. Ila unaonekana unaendelea kukua (umeshikilia nafasi ya tatu)
  • Halotel na Airtel wanaukuaji wa mzuri. Inaonekana nguvu ya ziada waliyoweka Halotel kuyafikia maeneo mengi mapya inaonekana kuwalipa – wameendelea kuwa na ukuaji mzuri kwa muda mrefu sasa.
  • Kwa ujumla wake mitandao yenye gharama nafuu zaidi ata kama mtumiaji hatumii kifurushi ni Halotel, TTCL, Smart (Benson) na Zantel.
  • Airtel Money inaongeza kwa ukuaji ukilinganisha na huduma zingine za kibenki za mitandao ya simu, idadi ya watumiaji ilikuwa kwa asilimia 12 katika kipindi hicho. Ukuaji wake na ule wa TIgo Pesa unaonekana kupunguza idadi ya watumiaji wa M-pesa (Vodacom).
SOMA PIA:  Matumizi ya simu janja pamoja na 'Drones' katika kupambana na Malaria

Vipi, je wewe una mtazamo gani juu ya matokeo haya? Unaweza kusoma ripoti nzima hapa – TCRA TelCom-Statistics-June-2017

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com