Mtandao wa Smile Kusambaa Zaidi Nchini: Kuja na Huduma za Kupiga Simu - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mtandao wa Smile Kusambaa Zaidi Nchini: Kuja na Huduma za Kupiga Simu

1
Sambaza

Mtandao wa Smile Tanzania ambao ni moja kati ya mtandao mkubwa kabisa unaotoa huduma ya intanet katika mfumo wa 4G umejipanga vyema kuanza kusambaza huduma yao katika maeneo mengi zaidi.
Wakiwa na takribani bajeti ya zaidi ya dola milioni 365 za kimarekani wanategemea kusambaza huduma zao katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Dodoma, Moshi, na Morogoro.

Mpango wao unajumlisha mpango wa kuwa na uwezo wa kutoa hadi huduma za maongezi ya simu kama ilivyo kwa mitandao mengine kabla ya mwisho wa mwaka 2016. Hayo yalisemwa na meneja mkuu wa Smile nchini Tanzania, Bwana  Eric Behner, wikiendi iliyopita katika shunguli waliyoiandaa kutambulisha rasmi mipango yao ya ukuaji.

INAYOHUSIANA  NMB, Halotel kutoa huduma za TEHAMA bure mashuleni

Kwa sasa mtandao wa Smile unatoa huduma zake za intaneti ya kasi ya 4G katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha tuu. Na ata kwa Dar es Salaam kuna maeneo mengi pembezoni mwa mji huduma yao inakosekana.

Hivi karibuni wametambulisha vifurushi vidogo zaidi.

Hivi karibuni wametambulisha vifurushi vidogo zaidi.

Kwa kiasi kikubwa ni jambo zuri wao kuzidi kukua na kuweza kuzidi kuleta ushindani katika utoaji huduma ya intaneti ya kasi zaidi nchini. Suala la bei za bando zake bado ni tatizo kidogo lakini ni vizuri kwao kuamua kuleta bando mpya za bei rahisi zaidi, bando wanazoziita Smile Lite.

here Je wewe unamaoni gani juu ya hili? Ushawahi kutumia intaneti ya mtandao wa Smile? Tuambie kuhusu kasi yake.

INAYOHUSIANA  Utoaji wa talaka kwa njia ya simu wakemewa

Soma Pia: Fahamu Tofauti Kuu Kati ya Teknolojia za 2G, 3G, 4G n.k

Vyanzo: IPPMedia na vyanzo vingine mtandaoni

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Smile kuja na huduma mpya - SmileVoice na SmileUnlimited

Leave A Reply