Mtandao wa Smile Wazidi Kujikuza katika Huduma za Teknolojia ya 4G LTE

0
Sambaza

Mtandao wa 4G wa Smile umezidi kujikita kuwekeza katika huduma zinazotegemea teknolojia ya 4G LTE, sasa watambulisha rasmi huduma za SmileVoice na SmileUnlimited.

Kama unakumbuka Septemba mwaka jana tuliandika kuhusu mafanikio yao ya kupata takribani dola milioni 365 kwa ajili ya kuzidi kuwekeza katika teknolojia ya 4G LTE hii ikiwa ni pamoja na kusambaza huduma hiyo kwenda sehemu mpya.

Smile tanzania

 

SmileVoice ni nini?

SmileVoice ni huduma ya kwanza Afrika inayofanikisha mawasiliano ya sauti kupitia teknolojia ya 4G LTE. App yao inayopatikana bure katika soko la Google Play na App Store inawapa uwezo watu wowote waliopakua app hiyo kwenye simu zao kuweza kupiga simu duniani kote.

Kwa watumiaji wa simu janja za Android au iPhone utaweza kupiga simu kwa urahisi na kwa kiwango kizuri cha sauti kutokana na mazungumzo hayo kusafirishwa juu ya teknolojia ya intaneti 4G LTE.

go to site Kuwa na app ya SmileVoice ni sawa na kuwa na laini nyingine ya pili kwenye simu yako. Badala ya gharama za mawasiliano kulipiwa kwa wastani wa sh/sekunde kupitia huduma ya SmileVoice inayotegemea data unalipia MB unazotumia katika upigaji wa simu husika.

INAYOHUSIANA  Adhabu kutokana na aina ya kosa la mtandao

SmileUnlimited ni nini?

SmileUnlimited ni kifurushi/bando jipya litakalomuwezesha mteja kupata huduma ya intaneti bure ndani ya muda wake wote wa bando husika – ila kasi ya intaneti hiyo itapungua baada ya utumiaji wa kiwango flani cha data.

Hadi sasa bei ya kifurushi hicho cha Unlimited bado hatujakijua, kikitambulishwa tutakutaarifu.

Mtandao wa Smile ni moja ya mitandao yenye nguvu sana katika eneo la teknolojia ya 4G LTE Tanzania, na nchi nyingine kadhaa za Afrika. Tayari wanamipango ya kuanza kufanya kazi nchini DRC – Kongo muda wowote kuanzia sasa.

get link Huduma za SmileVoice na SmileUnlimited zinategemewa kuingia pia katika nchi zingine ambazo tayari mtandao huo unatoa huduma, Nigeria na Uganda.

INAYOHUSIANA  Chaneli za ndani zaanza kurushwa bure

Vyanzo: Telecopaper, na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.