Mtandao wa Wikipedia wafungiwa nchini Uturuki

0

tecno phantom 8

Sambaza

Mtandao wa kutoa taarifa kuhusu mambo mbalimbali duniani wa Wikipedia wafungiwa nchini Uturuki baada ya kuchapisha taarifa iliyoikera Serikali ya nchi hiyo.

Taarifa hiyo ni ile inayoishutumu serikali ya Uturuki kushirikiana katika mambo ya kigaidi na vikundi kadhaa vya Kigaidi.

Wikipedia ilikataa kuondoa taarifa hiyo baada Uturuki kuitaka ifanye hivyo.

Wikipedia wafungiwa nchini Uturuki

Taifa la Uturuki: Wikipedia wafungiwa nchini Uturuki

Wizara ya uchukuzi na mawasiliano siku ya Jumamosi ya tarehe 29 aprili saa mbili asubuhi iliufunga mtandao huo na kufahamisha kwamba mtandao huo umefungwa nchini humo.

airtel ofa kabambe

Kufungiwa kwa Wikipedia kumeambatana na sheria ya makosa ya mitandaoni ya nchi hiyo iliyothibitishwa na Mahakama kuu ya nchi hiyo.

SOMA PIA:  Utafiti: Mitandao ya kijamii chanzo cha habari kikubwa kwa watu wengi

Serikali ya Uturuki imekuwa na udhibiti mkubwa wa taarifa zote zenye kuishutumu serikali yake inayoongozwa na Rais Erdogan, hasa hasa baada ya kuepuka jaribio la mapinduzi.

Si jambo la ajabu sana mitandao kufungiwa katika baadhi ya mataifa yenye sheria au utaratibu mkali kuhusu habari wasizozipenda au wasizoweza kuwatambua watumiaji wa mitandao hiyo vizuri pale wanapofanya makosa mitandaoni.

 

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com