Mteja Ashinda Kesi Dhidi ya Kampuni ya Simu - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mteja Ashinda Kesi Dhidi ya Kampuni ya Simu

0
Sambaza

mteja-simuMteja mmoja wa kampuni ya simu nchini Afrika ya Kusini ameshinda kesi aliyoshitakiwa na kampuni ya simu ya CELL C kwa kuweka bango/tangazo (billiboard) lililokuwa linaikejeli kampuni hiyo. Bango hilo lilokuwa linasema ya kwamba ‘CELL C ni moja ya kampuni isiyo na maana kabisa’.

Mteja huyo anadai alinunua simu mpya (pamoja na namba) na baadaye akajikuta ana deni la takribani laki 9 za kibongo kwenye huduma ya simu, akagundua deni hilo litakuwa linahusika na mteja aliyekuwa akimiliki namba hiyo kabla yake. Alipojaribu kuwaelezea wahudumu wa kampuni ya simu hiyo ili walitoe deni hilo katika rekodi zake alikataliwa, alijaribu njia nyingi sana na akaona amedharaulika na deni hilo kuendelea kuwa nalo.

Hapo ndipo akatumia takribani Tsh Milioni 10 kuweka bango la kuiponda kampuni hiyo ya simu. Baada ya kuombwa kulitoa bango hilo, Bwana George Prokas aliyeweka bango hilo alikataa na hapo ndipo kampuni hiyo ya simu iliamua kumburuza mahakamani, ikidai mteja huyo analichafua jina la kampuni hiyo. Mahakama ya Juu ya Gauteng imesema mteja huyo ana kesi ya kujibu, bango hilo linaingia kwenye haki yake kujieleza na imeitaka kampuni hiyo kumlipa mteja huyo gharama zote za uwakili alizotumia katika kesi hiyo – ambazo ni milioni kadhaa.

INAYOHUSIANA  Aina tatu tofauti za vimemeshi vyenye uwezo wa juu

Je ukiambiwa uweke bango kuhusu kampuni moja ya simu Tanzania, utaweka linalosemaje?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply