Muigizaji Jason Statham na Muimbaji Nicki Minaj Watengenezewa Magemu - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Muigizaji Jason Statham na Muimbaji Nicki Minaj Watengenezewa Magemu

0
Sambaza

Muigizaji wa filamu maarufu za The Transporter, Bwana Jason Statham na mwanamuziki maarufu wa kike, Nicki Minaj watatumika katika utengenezaji wa magemu spesheli yanayowahusisha. Mke wa mwanamuziki Kanye West, Kim Kardarshian tayari amepata mafanikio na pesa nyingi kutoka kwenye gemu lililotengenezwa likiwa na uhalisia wake linalofahamika kwa jina la Kim Kardashian: Hollywood.

Nicki Minaj na Jason Statham

Nicki Minaj na Jason Statham

Kampuni maarufu ya utengenezaji magemu ya Glu baada ya kuona mafanikio waliyoyapata na Kim Kardashian sasa imeingia mkataba na Jason na Nicki Minaj

Gemu la Kardashian lilifanikiwa kuwa moja ya magemu yanayoingiza mapato mengi sana katika muda mfupi tuu tokea lianze kupatikana. Na wengi walisema ni gemu ambalo mashabiki wake wengi wangeshinda kuliweka chini baada ya kuanza kulicheza. Mafanikio hayo makubwa kwa Kim Kardashian ndiyo yaliyosababisha watengenezaji magemu wengine waone umuhimu wa kuwatumia watu mashuhuri kama Jason Statham na Nicki Minaj wakitegemea magemu hayo pia yaweze kufikia mafanikio makubwa pia.

INAYOHUSIANA  Mechi za La Liga kuonyeshwa bure na Facebook

Gemu la Jason Statham

Muonekano na sauti yake vitatumika katika gemu la upiganaji yaani la Action linalofahamika kwa jina la Sniper X: Kill Confirmed. Gemu hilo litapatikana katika simu na tableti zinazotumia programu endeshaji za Android na iOS.

Gemu la Nicki Minaj

Sauti, muonekano na masuala yake ya ubunifu yatatumika katika gemu ambalo wengi wanaona linaweza likafanana kwa kiasi flani na la Kardashian. Yaani litahusisha maisha ya kila siku ya mwanamziki huyo. Gemu hilo litapatikana katika simu na tableti zinazotumia programu endeshaji za Android na iOS.

Soma Pia – Kim Kardashian: Hollywood – Gemu linaloingiza Tsh BILIONI 1.1 Kila Siku

INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

Magemu hayo yanategemewa kuanza kupatikana katika kipindi cha kati ya mwezi wa 12 mwaka huu na wa tano mwakani.

order flagyl cheap Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia kila siku.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply