Muonekano mpya wa Instagram: Mabadiliko ya Muonekano Yafanyika! #Apps

0
Sambaza

Muonekano mpya wa Instagram waja rasmi. Tuliandika hivi karibuni kuhusu Instagram kuja na muonekano tofauti, jambo hilo sasa ni rasmi na huu ndio muonekano wake mpya.

Walichojitahidi Instagram ni kutoacha historia yao kuu katika muonekano wao mpya. Kutokana na mabadiliko makuu ya mfumo wa muonekano katika Apple, yaani iPhone na iPad, pamoja na Android na ujio wake wa Material Design…moja kwa moja app ya muonekano wa app ya Instagram ukaanza kuonekana kutofanana vizuri na programu endeshaji hizo.

SOMA PIA:  Dola Bilioni 24! Snapchat yazidi kujidhatiti katika soko la hisa

Kuanzia kwenye ‘icon/logo’, yaani alama kuu mabadiliko yamefanyika. Angalia picha hii chini.

Muonekano mpya wa Instagram 2016

Muonekano mpya wa Instagram

Kushoto alama za zamani na kulia za sasa

Mabadiliko ya kimuonekano wa ndani ya app ipo kama hivi…kushoto ni muonekano wa zamani na kulia ni wa sasa.

Muonekano mpya wa Instagram

Muonekano mpya wa Instagram kulia

App ya Instagram ni moja ya app muhimu sana kwa familia ya apps zinazomilikiwa na kampuni ya Facebook. Kwa sasa app ya Instagram inawatumiaji takribani milioni 400 na watumiaji hawa wanaupload video na picha takribani milioni 80 kila siku.

SOMA PIA:  Rais wa Urusi Vladimin Putin hatumii kabisa simu janja

Ingawa labda kuna faida chache kwa muonekano huu bado inaonekana watumiaji wa muda mrefu wa app hii hawatapendezwa na mabadiliko haya. Je vipi kwako? Unapendezwa na mabadiliko haya?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com