Matumizi ya betri kwenye simu janja/vifaa vya kidijiti yanachagizwa kwa kiasi kikubwa na kiasi cha mwanga ambao unakuwa umeweka kitu ambacho kinasabisha kuhitaji kimemeshi ili kuchaji.
Makampumi mbalimbali yanakuja na kipengele ambacho kitaruhusu kuwa na muonekano wa giza kitu ambacho tayari tumeshakiona kwenye Youtube na hata kuwa mbioni kuwekwa kwenye WhatsApp.
Kwa mujibu wa utafiti waliofanya Google na kukiri kuwa muonekano wa giza unasaidia kutunza ubora wa betri na kuongea kuwa ingawa mwanga mkali/mdogo kwenye simu unaathiri matumizi ya betri lakini pia rangi ambayo mtu amechagua kuwepo kwenye uso wa juu pia inachangia kumaliza umeme wa betri.
Kwa vifaa vyenye kioo cha AMOLED kitakuwa msaada zaidi kwenye utunzaji wa betri kwenye muonekano wa giza kulinganisha na bidhaa ambazo zina kioo cha LCD.
Kwenye Youtube kipengele cha muonekano wa giza ndio kinaonyesha dhahiri ni kwa kiasi gani kifaa husika kinatumia betri ikiwa na muonekano wa giza au ule wa kawaida ambao wengi ndio tunaoufahamu.
Inashauriwa sana kutoweka kiasi cha mwanga mpaka mwisho lakini pia kutotumia rangi za mng’ao ili kufanya betri la kifaa gusika kuweza kudumu na umeme.
Vyanzo: GSMArena, The Verge