Mwanamke kujifungua 'mjukuu wake'! #Afya #Teknolojia - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mwanamke kujifungua ‘mjukuu wake’! #Afya #Teknolojia

0
Sambaza

Mwanamke ambaye anataka kutumia mayai ya uzazi ya bintinye ili kumzaa mjukuu wake ameshinda kesi mahakamani na kuruhusiwa kufanya hivyo.

Mwanamke huyo wa umri wa miaka 60 alikuwa amekatazwa kupeleka mayai ya bintiye kwenye kliniki moja nchini Marekani hali iliyosababisha akate rufaa. Bintiye ambaye aliaga dunia mwaka 2011, anaripotiwa follow url kumuambia mamake amzalie watoto wake lakini mamake alishindwa katika kesi mwaka uliopita.

Hata hivyo aliruhusiwa kupinga hukumu hiyo katika mahakama ya rufaa. Mwaka 2014 halmashauri inayohusika na mayai ya uzazi, ilisema kuwa enter mayai hayo yasingeruhusiwa kutoka mjini London kwa sababu bintiye hakuwa ametoa idhini kamili kabla ya kifo chake.

mayai

Lakini kwenye kesi ya sasa mawakili waliwaambia majaji kuwa, mwanamke huyo alikuwa anataka kutimiza matakwa ya bintiye ya kuzaa mtoto akitumia mayai yake na kisha amlee mtoto huyo.

Kwa sheria za Uingereza  http://trinityhpastor.org/tag/concupiscence/ hakuna ukomo wa umri kumzuia mwanamke kupandikizwa mayai ambayo yalikuwa yametunzwa na hatimaye kuweza kuzaa baada ya miezi ya kujifungua kutimia.

INAYOHUSIANA  Uchina kutengeneza vipuri vyake mwenywewe

Nia ya mwana mama huyo kuyapeleka mayai hayo New York Marekani ni  kwenda kutafuta mbegu ya kurubisha mayai hayo na kisha kupandikizwa kuweza kubeba na kulea mimba hiyo.

Mayai ya mwanamke yakiwa yamehifadhiwa mwanamke kujifungua

Mayai ya mwanamke yakiwa yamehifadhiwa

Je, unadhani mwanamke huyo atashinda rufani yake kutokana na maelezo yake? Endelea kufuatilia Teknokona nasi tutazidi kuwataarifu.

Makala hii imeandikwa kwa usaidizi wa vyanzo mbalimbali: BBC, The Telegraph na Women’s health.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.