Mwanzilishi mwenza wa Apple aamua kuikacha iPhone X

0
Sambaza

iPhone X ndio simu pekee ambayo bado haijanza kuuzwa ingawa tayari imekwishazinduliwa pamoja simu janja nyingine kutoka Apple. Bw. Steve Wozniak amesema hatonunua simu hiyo mara tu zitakapoanza kuuzwa kutokana na kutomvutia.

Kwa wasio fahamu, Bw. Steve Wozniak ndiye mwanzilishi mwenza (baada ya marehemu Steve Jobs) wa kampuni ambayo mpaka hivi leo inasifika sana katika biashara ya vifaa vya kiteknolojia (simu, saa, kompyuta, n.k).

Uamuzi wa Bw. Steve Wozniak umekuja baada ya kuona simu janja ya iPhone X haina tofauti kubwa na iPhone 8 hivyo haoni sababu ya kumiliki iPhone X mara tu zitakapoanza kuuzwa mnamo Novemba 3 (unaweza kuanza kuagiza kuanzia Oktoba 27 2017).

Muonekano wa iPhone X ambayo simu hiyo haina kitufe cha nyumani, ina teknolojia ya kutumia uso na mengineyo mengi tu.

Historia fupi ya Bw. Steve Wozniak na Apple kwa ujumla.

Apple (kampuni) ilianzishwa mwaka 1976 na Bw. Wozniak na Steve Jobs. Wawili hao walishirikiana bega kwa bega katika uundaji wa vifaa vya kiteknolojia na kuifanya Apple kuwa na jina na kuwa moja ya kampuni bora zaidi kwenye masuala ya kiteknolojia.

Bw. Wozniak alihusika sana kwenye uundaji wa bidhaa husika za mwanzo kabisa za wakati huo huku marehemu Jobs yeye akiwa na uono wa mbali wa bidhaa husika kuwa itafanya vyema pamoja na kuitangaza bidhaa yenyewe.

Mwaka 1985, Bw. Wozniak aliachana na Apple baada ya kutopendezwa na mwenendo wa kampuni kwa wakati huo lakini amekuwa mmoja ya watu ambao wananunua bidhaa za Apple mara tu zinapotoka. Kujua mengineyo kuhusu Bw. Steve Wozniak BOFYA HAPA!

Bw. Wozniak (kushoto) na Jobs (kulia) wakiwa kwenye uundaji wa moja ya kompyuta za kwanza za Apple miaka ya 1970.

Mwanzilishi huyo mwenza wa Apple ana amini kuwa simu janja nyingi za siku hizi zimekosa msisimko kama ilivyokuwa zamani kutokana na simu hizo kuwa na tofauti ndogo mathalani yeye (Wozniak) anaona iPhone 8 ipo sawa na iPhone 7, iPhone 6 😯 😯 .

SOMA PIA:  Drones za Amazon zinazotumika kusambaza vitu kwa wateja

HIvi sasa si shabiki sana wa simu janja kama miaka ya nyuma na anaangazia zaidi teknolojia za ndege zinajiendesha zenyewe, magari yanayotumia nishati ya umeme, magari yanayojiendesha yenyewe na wanachofanya kampuni hizo.

Vyanzo: NBC, Telegraph

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com