Kama ni mfuatiliaji mzuri wa TeknoKona basi utagundua kuwa habari hii iliandikwa toka mwanzo na kwa sasa nakupa mawili matatu juu ya pale ilipofikia.
Soma Hapa ili kujua kiliandikwa nini awali.
Kampuni ya Essential Products Inc ambayo inamilikiwa na mmoja kati ya waanzilishi wa Android, Andy Rubin imesema kuwa ina kitu cha aina yake katika stoo na ina mpango wa kukuionyesha tarehe 30 mwezi wa tano.
Leo sitakua muongeaji sana maana hata mimi nina shauku kubwa ya kukijua kitu hicho. AKili yangu yote inanituma kuwa itakua ni simu janja tuu kulingana na viashiria vilivyo.
Kampuni ya Essential Products Inc katika uwanja wake wa Twitter iliandika mambo mengi huku dhima yake kubwa ni kuwaweka watu wawe tayari kwa mapokezi juu ya chochote watakacho kitoa tarehe 30 hiyo
Hi, welcome to our Twitter page. We're here to let you know something big is coming May 30th! Stay tuned…
— Essential (@essential) May 25, 2017
Andy Rubin nae alichangia kidogo katika uwanja wake wa Twitter kwa kuwaambia watu wakae tayari na kuanza kufuatilia kurasa za @essential kwa kupata habari za hapa na pale juu ya kile kitakachojiri.
https://twitter.com/Arubin/status/867782330173095937?ref_src=twsrc%5Etfw&ref_url=http%3A%2F%2Fwww.techtimes.com%2Farticles%2F208276%2F20170525%2Fessential-smartphone-could-be-unveiled-soon-as-android-cofounders-company-teases-something-big-on-may-30.htm
Baada ya hapo tena kampuni ilituma picha katika mtandao wa Twitter. Picha hii kwa haraka haraka ni ya simu janja lakini kuna vitu vingi vya kujiuliza juu ya simu hii kama vile umbo lake
Lakini ni vigumu kujua kila kitu kwani simu hii ilikua imefunikwa na weusi ulikua umetanda. Cha muhimu ni kusubiri mpaka siku ambayo kampuni imetuambia tusubiri.
Kwa haraka haraka ni kwamba simu janja hii inaweza ikawa ina kamera ya ajabu kidogo.. yaani ile ya nyuzi 360 ambayo inachukua kila upande,