Raia wa Czech Republic, Jakub F (30) anakabiliwa na hukumu ya mahakama kwa kufanya wizi wa mtandaoni. Cha kushangaza kwenye hukumu yake, Jacob anaweza kuachiwa huru endapo filamu inayopingana na wizi wa aina ya alioufanya itapata kuonekana kwa watu mara 200, 000.
Uamuzi huu ulitokea baada ya makubaliano ya nje ya mahakama yaliyohusisha makampuni kadhaa yaliyoumizwa na uhalifu wake, baada ya kubaini kwamba Bw. Jakub hawezi kuwalipa. Sharti la kuonekana kwa video hiyo mara 200, 000 ndani ya mwezi mmoja baada ya video kuachiwa linatazamiwa na makampuni hayo kumfanya Jakub ausambaze ujumbe wao kwa juhudi zote. Kinyume na kutimiza sharti hilo, makampuni hayo yatakuwa na uhuru wa kumshtaki tena kwa kesi kubwa zaidi.
Wizi wa mtandaoni unasababisha kiasi cha wastani, cha zaidi yaTshs billion 15 kwa makapuni duniani. Jakub amewekwa pia kwenye mtandao na kukaririwa akisema “Nilidhani ya kwamba nilikuwa sifanyi makosa. Sikudhani ya kwamba nilikuwa nayaumiza makampuni makubwa… Nilijiridhisha ya kwamba mimi ni samaki mdogo sana kwenye bahari kubwa. Video iliyotengenezwa inaonesha Jakub hakutumia programu kwa kujipatia kipato, na inawaonya wezi wengine wa mtandao ya kwamba wanaweza kukamatwa. Imeripotiwa kwamba Jakob aliweka Microsoft Windows 7 na 8, pamoja na programu nyingine kwenye mitandao ya kusambazia.
Video hiyo sasa imeonekana zaidi ya mara 1, 000, 000 na inaitwa – “The Story of My Piracy” na Jakub ndiye mwigizaji mkuu.
Chanzo: BBC Technology
No Comment! Be the first one.