Mwizi wa simu 100 na zaidi akamatwa kisa app ya Find My iPhone

1
Sambaza

Janga la wizi wa vitu kama simu linazidi kukua duniani kote kakini hata hivyo teknolojia imeonekana kuwa msaada mkubwa. Siku hizi ukiwa makini kufuatilia mali yako iliyoibiwa unaweza ukaipata kwa msaada wa teknolojia mbalimbali.

Kuibiwa simu hasa simu janja ambazo kiuhalisia si bei rahisi ni jambo linafedhehesha sana kutokana na kwamba mambo mengi sana tunaweza tukahifadhi kwenye simu zetu na kuepuka kubeba vitu vingi kwa wakati mmoja pasipo na ulazima.

Mshukiwa wa wizi ambaye inaaminika alikuwa ameiba zaidi ya simu 100 aina ya iPhone amekamatwa nchini Marekani. Simu hizo zilikuwa zimeibiwa katika tamasha la muziki la Coachella katika jimbo la California. Mwizi huyo alikamatwa baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kutumia programu tumishi ya Find My iPhone kufuatilia simu zao wakiwa bado kwenye eneo la tamasha hilo.

Simu mbalimbali aina ya iPhone ambazo zilikuwa zimeibwa

App ya Find My iPhone App hiyo huonesha ilipo simu ya mtu (kwa simu za iPhone), na baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kufuatilia kutumia app hiyo hadi wakamnasa mshukiwa.

SOMA PIA:  PowerShake: Teknolojia ya kushare chaji kwa kutumia Wi-Fi #Maujanja

Jamaa hiyo mwenye jina la Reinaldo De Jesus Henao alikamatwa na simu zingine zaidi ya 100 zikiwa ndani ya begi lake la mgongoni.. Yaani jamaa alienda kwenye tamasha hilo akiwa kajipanga kuzibeba simu za watu wengi zaidi awezavyo. Baada ya kumkamata baadhi ya simu zilirejeshwa kwa wenyewe mara moja kwa wale waliokuwa bado wapo eneo la tukio.

Jinsi ya kuchukua tahadhari

Tunapokwenda sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu mambo mengi yanaweza kutoka ikiwemo upotevu wa mali na kwa kesi kama ya wizi wa simu na vitu vingine vinavyoweza kuibwa kiurahisi unaweza ukachukua tahadhari kwa kufanya yafuatayo:-

  • Kutoweka vitu vyao vya thamani katika mifuko yao ya nyuma
  • Kuhakikisha vitu vyao vya thamani huviweki pamoja
  • Kubeba pochi bandia ili kuwahadaa wezi
SOMA PIA:  YouTube yafanya mabadiliko ya logo!

Soma pia;

Je, wewe ulishawahi kuibiwa na kufanikiwa kupata mali yako? Ulitumia mbinu gani kupata hicho ulichokuwa umeibiwa? Tuambie katika sehemu ya maoni hapo chini.

Vyanzo: BBC, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com