Nafasi za Kazi kuanzwa kutangazwa kupitia Facebook

0
Sambaza

Katika hali inayoonesha mtandao wa kijamii maarufu unataka kushindana moja kwa moja na LinkedIn, mtandao maarufu wa masuala ya ajira na urafiki wa kikazi na kibiashara.

follow url facebook

Mabadiliko ambayo yapo njiani kwenye mtandao huo wa Facebook yatazipa Pages (Kurasa) za kibiashara na makampuni uwezo wa ku’post nafasi za Ajira kwenye kurasa zao.

http://protestchildkilling.com/red-rose-rescue-father-stephen-speaks-of-his-time-in-jail/ Kuna uwezekano Facebook ata wakatoza makampuni pesa ili nafasi hizo za ajira zionekano kwa watu wengi zaidi.

Nafisi hizo za ajira zitaweza kuonekana kupitia eneo la pembeni kwenye page hizo maarufu kwa jina la ‘Tabs’. Hili ni eneo linalokupa uwezo wa kwenda moja kwa moja kwa vitu kama vile Video, Picha, na taarifa zingine zilizopo kwenye ukurasa husika wa Facebook. Kuelewa zaidi angalia picha hii;

facebook ajira

Eneo la utafutaji Ajira kwenye kurasa za Facebook

Mtandao wa LinkedIn ambao tayari una umaarufu mkubwa katika eneo la mahusiano ya kiajira na utafutaji nafasi za kazi bado upo sehemu nzuri sana na inawezekana kwa kiasi kikubwa hawataathirika na maboresho haya kutoka Facebook. 

LinkedIn pia umenunuliwa hivi karibuni na Microsoft, hivyo kuna uwekezaji mkubwa unaendelea na wapo katika eneo zuri kiushindani kiasi ya kutoathirika na ujio wa maboresho haya kutoka Facebook.

Je una mtazamo gani juu ya maboresho haya yatakayofanywa na Facebook?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia;

FacebookTwitterInstagramYouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Vinara wa matumizi ya sarafu zisizoshikika
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.