Namna ya kuhamishia App katika Memori kadi! #Maujanja

0
Sambaza

Kuna tatizo la kujaa App kwa baadhi simu ambazo hazina Diski ujazo (Internal Storage) kubwa hivyo kupelekea usumbufu kwa watumiaji wengi ambao mahitaji ya kuwa na App nyingi kwao ni muhimu.

Tatizo la kujaa upesi kwa Diski ujazo ni kero sana kwa watumiaji wa simu, lakini hili kwa wakati wa nyuma hakukuwa na njia mbadala zaidi ya kupunguza zilizokuwemo.

MEMORI KADI

Lakini hilo kwa sasa linawezekana kuweka App nyingi kwa namna uitakayo hata kama Diski ujazo yako ya simu ni ndogo. Linawezekana kwa kutumia memori Kadi (Micro SD Card)

SOMA PIA:  Wadukuzi 10 hatari zaidi wa kompyuta duniani!

Wakati wa nyuma kulikuwa hakuna namna ya kuweka App katika Memori kadi. Lakini nyakati za sasa hilo linawezekana kwa simu za Android. Ni kwa baadhi ya simu hususani kuanzia zile zenye toleo la Lollipop (Android Version  5.0) na kuendelea.

Jambo hilo linaweza kukufanya ukainstall App nyingi zaidi katika simu bila ya wasiwasi wowote. Lakini kumbuka unapoweka App katika Memori Kadi usijaribu kuitoa ndani ya simu, kwani kufanya hivyo utashindwa kuzitumia App hizo.

SOMA PIA:  Ujenzi wa Darubini kubwa zaidi duniani waanza.

Jambo hili itategemea sana na aina ya Memori Kadi utakayoitumia. Ni vizuri kuweka iliyo na nafasi kubwa zaidi. Kuanzia 10 GB na kuendelea itakupa nafasi nzuri ya kuweka App nyingi uzipendazo.

Hatua ambazo zitakuwezesha kuhamishia App zote katika Memori kadi ni kama ifuatavyo.

  1. Nenda setting
  1. Kisha App (Baadhi ya simu panasomeka application manager/Manage Apps nk)
  2. Ukishaingia App manager Utaona App ulizoinstall katika simu yako
  3. Chagua App utakayopenda kuihamishia katika Memori Kadi
  4. Ukishaichagua App utauona sehemu pameandikwa ‘move to SD Card’, ni kiasi cha kubonyeza tu na App itahamia huko.
SOMA PIA:  App ya Youtube kwenye Android imefanyiwa maboresho ili kuvutia zaidi

Kwa ambao wanatumia toleo la Android Nougat 7.0 na kuendelea wanaweza kuseti moja kwa moja kwenye Memori Kadi kila wakiinstall App inakwenda katika Memori Kadi.

Muhimu kutokuitoa Memori Kadi yako katika simu. Ukiitoa hutaweza kuzitumia App ulizozihamishia huko mpaka utakapoiingiza tena katika simu.

Kumbuka zoezi hili kwa baadhi ya simu za Tecno haliwezekani.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com