Nani Mtawala Katika App Za Ku Chati Kwa Sasa? - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Nani Mtawala Katika App Za Ku Chati Kwa Sasa?

0
Sambaza

preview

Wiki hii ni maadhimisho ya mwaka mmoja kwa Facebook tangia wanunue mtandao wa WhatsApp kwa dola bilioni 19 za kimarekani. Kampuni hilo liko wapi kwa sasa?. Ukiachana

watch

na facebook kuna makampuni makubwa mengine ambayo yanawawezesha watu kuchati kama vile Twitter, Snapchat na mengineneyo mengi. Licha ya yote haya nani mtawala?

Kutuma/Kupokea meseji kwa ujumla ndio kumekua ni moja kati ya uwanja mkubwa na unaokua kwa kiasi kikubwa sana hivi sasa katika sekta ya mawasiliano. Hapa haijalishi ni kampuni gani inasaidia kufikisha ujumbe huo ( mfano Facebook, Twitter, Tango, WeChat na WhatsApp) kwa kuwa unaongelewa ujumbe kwa ujumla. Inasemekana watu hawapigi simu tena kama zamani, Ndio! wanapendelea kuchati.

Ndani ya WeChat, Line na Tango kuna Magemu, App ndani ya Mesenja (kama vile huduma  ya ‘ride-sharing’, kuagiza chakula, muziki na huduma nyingine nyingi). Watu wanaishi ndani ya hizi App kwa kufanya vitu vingi ambavyo mtu anaweza fanya kwa kutumia App nyingine inayojitegemea ndani ya simu-janja zao katika maisha yao ya kila siku.

INAYOHUSIANA  Snapchat waonja shubiri ya kupata hasara

source url Nani Anashinda……

Dola bilion 19 ikiwa na bei ambayo WhatsApp iliuzwa ilikua na bado inabaki kuwa juu kuliko App zingine. Lakini tuweke pesa kando, Upatikanaji huo  unaleta maana. Facebook wanaonekana kuweka kando kwa sasa wazo lao la kutengeneza simu janja zao. Sasa unafanyaje kama huwezi kushindana katika Vifaa (Hardware)? Unashindana katika Software!. Google waliliona hili walipopata Android mwaka 2005 na  Facebook imefanya hivyo hivyo baada ya kupata makampuni kama vile WhatsApp na Instagram

Facebook sasa wana App 4 kati ya zile 11 bora katika iOs AppStore (Facebook Messenger, Facebook, Instagram, na WhatsApp) na 4 katika zile app 21 bora katika soko la Android Google PlayStore kwa hiyo wakati Apple wanamiliki simujanja Facebook wanamiliki nini unachoweza fanya na simujanja. Hapo Umeelewa Sio?

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Wamiliki/Viongozi wa kundi kuamua nani atume ujumbe

Januari WhatsApp iliripotiwa kuwa na watumiaji milioni 700 wa mwezi wa kudumu na kutuma meseji bilioni 30 kwa siku wakati Global SMS (text msgs) zinatumwa kwa makadirio ya bilioni 20 tuu kwa siku. Facebook wamejijengea mtandao wa kijamii bora ambao unatumika hadi sasa duniani kote lakini wana uhakika gani watazidi kubaki kuwa juu na ukizingatia facebook haipendwi sana siku hizi na vizazi vipya?

buy ciprofloxacin online canada Social media buttons…….Na Nani Anaweza Kuishinda Facebook?

Kama Facebook itaendelea na mfumo wake huu huu wa kufanya kazi, inaweza ikashushwa na kampuni ambalo liko tayari kuchukua riski kubwa katika soko.Kwa mfano Tencent, ni mojawapo kati ya makampuni makubwa yanayo chapisha magemu (na pia moja kati ya mtandao mkubwa wa kijamii) na pia asilimia 70 ya mapato yao yanapatikana katika magemu. Mara kwa mara wananunua au kuwekeza katika makampuni ambayo yana manufaa kwao hata wakichanganya ujuzi wao na wa kampuni jingine walilowekeza wanapata faida na pia hawakusita kutengeneza mtandao wa kijamii wa WeChat

INAYOHUSIANA  Microsoft na WhatsApp waunganisha nguvu kufanya kitu

Kuna Makampuni mengi yanaweza ishinda facebook yakikaza buti tuu mfano Twitter, Snapchat, WeChat, Kik na mengine mengi. Ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Twitter, Facebook Na Instagram

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply