Natural Cycles: App ya kuwasaidia watu kuepuka mimba zisizotarajiwa yasababisha mimba kibao

1
Sambaza

App maarufu ya kusaidia kujikinga na mimba zisizotarajiwa inayokwenda kwa jina la Natural Cycles imejikuta kwenye kipindi kigumu baada ya madai ya kwamba haipo sawa.

App ya Natural Cycles ni app ya kwanza duniani kupata sifa ya kutumiwa kama njia ya kuzuia upatikaji mimba baada ya kupata kibali mwezi Februari 2017. Kibali hicho kilichotolewa Ujerumani kimemaanisha utumiaji wa app hii ni wa kiwango kimoja ukilinganisha na njia zingine za kuzuia mimba kama vile utumiaji wa kondom, dawa za vidonge, n.k.

natural cycles

Sifa yake imeanza kuhojiwa baada ya wanawake 37 waliokuwa wanatumia app hiyo huko nchini Swideni katika jiji la Stockholm kupata mimba ilihali walikuwa wanatumia app hiyo. Hawa ni kati ya wasichana 668 wanaotumia app hiyo waliokuwa chini ya uangalizi wa hospitali moja mjini hapo.

SOMA PIA:  Tweet ya Obama ya 'kuvumiliana' imepata 'Like' nyingi zaidi katika historia ya Twitter

Malalamiko rasmi ya kudai uchunguzi yametolewa na hospitali ya jijini humo, Hospitali ya Södersjukhuset, kwenda kwa shirika la udhibiti wa viwango la nchini humo, Swedish Medical Products Agency.

App hiyo inafanyaje kazi?

Ina scan joto la mwili la mwanamke na kisha kusasisha taarifa kuhusu siku ambazo mtumiaji anaweza kupata ujauzito – taarifa zinakuwa kwenye app iliyokwenye simu. Huweka taarifa zote muhimu katika mfumo wa kalenda, na kuonesha siku hatari (ambazo mtumiaji anaweza kupata ujauzito kama atashiriki tendo bila kutumia kinga au njia nyingine ya kuzuia mimba zisizotarajiwa).

natural cycles

App ya Natural Cycles itapata data za joto mwili la mwanamke kupitia kifaa cha kipimajoto/thermometer spesheli kutoka kwao.

Kampuni inayotengeneza app hiyo imejitetea na kusema ukilinganisha idadi ya watumiaji wa app hiyo wanaodai ya kwamba wamepata ujauzito na idadi ya watumiaji maelfu wanaotumia app hiyo basi bado inaonesha app hiyo inafanya kazi kwa kiwango kikubwa tuu hata ikilinganishwa na njia zingine za uzazi ambazo pia sio za uhakika kwa asilimia 100.

SOMA PIA:  Mwizi wa simu 100 na zaidi akamatwa kisa app ya Find My iPhone

Kupitia mtandao wao wanasema huduma yao ya Natural Cycles ina uwezo wa asimilia 93 katika kusaidia kuzuia mimba zisizotarajiwa. Na pia ni njia ambayo hausishi madhara yeyote kwa mtumiaji wake, kwani zaidi ya joto tuu hakuna kingine anayeitumia anafanya.

Huduma ya Natural Cycles ni bure mwezi wa kwanza, kisha ni dola 9.99 za Kimarekani kwa mwezi (zaidi ya Tsh 20,000/=).

Vipi una maoni gani juu ya njia za kisasa za kiteknolojia zinazotaka kusaidia katika kurahisisha huduma ambazo tumekwishazizoea katika njia/mfumo mwingine?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com