Nchini Ufilipino mitandao mbalimbali ya video za ngono yafungiwa

1
Sambaza

Mitandao maarufu duniani kwa video za ngono yafungiwa nchini Ufilipino.  Orodha ya mitandao hiyo ni pamoja na XVideos, Redtube na Pornhub.

video za ngono ngono yafungiwa

Tovuti za ngono ni moja ya mitandao inayotembelewa zaidi duniani kote

Shirika la kiserikali linalosimamia sekta ya mawasiliano nchini humo limethibitisha maamuzi hayo kwa CNN ya kwamba wametoa amri kwa makampuni ya mawasiliano nchini humo (ISP) kuzuia upatikanaji wa mitandao hiyo kwa wateja wao wote kufikia Januari 14.

Hadi leo inasemekana tayari baadhi ya watoa huduma wakubwa nchini humo wameshaanza kufanyia kazi agizo hilo. Mitandao ambayo tayari washafanya hivyo ni pamoja na mtandao wa Smart na Sun Cellular ya nchini humo.

PornHub ni moja ya tovuti inayotembelewa zaidi nchini humo

Hivi karibani mtandao maarufu kwa video za ngono wa Pornhub ulitoa ripoti kuhusu watumiaji wake na kuonesha data zinazoonesha watumiaji kutoka nchini Ufilipino kwa wastani wanatumia dakika 12 na sekunde 45 kwenye mtandao kila wanapotembelea, kiwango hichi ni cha juu kabisa duniani kote.

SOMA PIA:  Namna ya kuzima Video zinazocheza zenyewe Facebook katika simu na Kompyuta

Labda pia suala hili ndilo lililoamsha uamuzi wa serikali. 🙂

Je unamtazamo gani juu ya upatikanaji wa mitandao hii nchini Tanzania?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Chanzo: BBC na tovuti mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com