Ndege yacheleweshwa kutokana na ‘Hotspot’ yenye jina la Galaxy Note 7

0
Sambaza

Kitendo cha mteja mmoja nchini Marekani kutumia Samsung Galaxy Note 7 kama jina la hotspot ya wi-fi kwenye simu yake ilisababisha ndege ya Virgin kucheleweshwa kwenye kiwanja cha ndege.

Simu za Samsung Galaxy Note 7 zimepigwa marufuku kubebwa kwenye ndege na serikali nyingi duniani kote baada ya kuwa na matatizo yaliyokuwa yanasababisha simu nyingi kulipuka.
Ndege yacheleweshwa

Muonekano wa wifi hotspot ndani ya ndege hiyo, picha hii ilipigwa na mmoja wa wasafiri

Baada ya kuonekana kwa hotspot hiyo wahudumu wa kwenye ndege hiyo waliomba mteja yeyote mwenye simu hiyo ajitaje mara moja ili waitoe simu hiyo. Baada ya kuona hakuna majibu kampteni wa ndege hiyo alisema yuko radhi kusimamisha safari hiyo kwa muda mrefu zaidi kuhakikisha kila begi na abiria anasachiwa hadi kuhakikisha simu hiyo inapatikana.
Kuona hivyo mtu mwenye simu aliyeweka jina la wifi hotspot Samsung Galaxy Note 7_1097 alijitokeza na kuomba kujieleza akisema hakuna simu hiyo bali ni yeye ndiye mwenye simu ambayo ata si Galaxy Note 7.

Simu za Samsung Note 7 zishalipuka na kusababisha hasara katika sehemu mbalimbali, gari hili aina ya Jeep liliungua nchini Marekani pale mwenye gari alipoacha simu yake ikiwa inachaji ndani ya gari hilo

‘Mabibi na mabwana, tumeipata simu. Kwa bahati nzuri simu hiyo imebadilishwa tuu jina kwenye Galaxy Note 7, ila si ya Note 7’ – Mhudumu wa ndege alitangaza.
Inasemekana abiria huyo hakuchukuliwa hatua yeyote na safari ikaendelea.
Simu za Samsung Galaxy Note 7 zilikubwa na balaa la milipuko ambayo hadi sasa sababu kuu bado haijatolewa ila wengi wanaamini ni tatizo la kiufundi na kiubunifu zaidi baada ya juhudi za kufanya simu hiyo iwe nyembamba zaidi.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Chanzo: BBC na tovuti mbalimbali

SOMA PIA:  Nokia 8 Sirocco: Simu janja matata, yenye kava imara
Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com