Ndege zisizokuwa na marubani “Drones” kuanza kutumika huko Dubai

0
Sambaza

Drones ambazo zimekuwa zikitumia katika mambo mengi katika miaka ya hivi karibuni ikiwemo uchuakuaji wa picha za mnato, kutumika katika vita, n.k sasa teknolojia hiyo imechukua sura mpya.

Ndege isiyokuwa na rubani ambayo inaweza kuwabeba watu, itaanza kutumiwa kwa uchukuzi wa abiria Dubai mwezi Julai. Ndege hiyo muundo wa eHang 184 kutoka China tayari imefanyiwa majaribio.

Ndege hiyo inaweza kubeba abria mmoja wa uzani wa kilo 100 na inaweza kupaa kwa dakika 30 kwa wakati mmoja.

Yanayohusu ndege aina eHang 184

  • Ndege hiyo ina skrini ya kompyuta ambapo mtu anaweza kubofya na kuchagua anataka kwenda wapi. Mtu anauwezo wa kuwa na uzito wa hadi kg 100
  • Hamna mitambo mingine yoyote ya kutumiwa na mtu kudhibiti ndege hiyo kutoka ndani.
  • Ina kiwango cha betri cha kuiweka angani kwa dakika 30
  • eHang 184 inaweza kupaa kwa kasi ya maili 100 kwa saa (kilomita 160 kwa saa) na inaweza kusafiri umbali wa kilomita 50 baada ya betri yake kujazwa chaji. Kwa juu inaienda juu hadi urefu wa takribani mita 300.
  • Ndege hiyo ya thamani ya $14m (zaidi ya Tsh. 308bn)

      Ndege aina ya eHang 184 isiyotumia rubani.

eHang 184 iliidhinishwa baada ya kufanyiwa majaribio Nevada nchini Marekani Juni 2016. Hata hivyo mhadhiri wa ngazi ya juu wa masuala ya uchukuzi wa ndege katika Chuo Kikuu cha England Magharibi alidokeza kwamba angependa kuona kwamba ndege hiyo ikipaa kwa zaidi ya saa 1,000 kwanza kabla ya binadamu kuingia ndani.

SOMA PIA:  Hizi ndiyo Fomu za Maombi ya Kuendesha ndege Zisizokuwa na Rubani (Drones)

Mwezi uliopita, kampuni ya Israel ya Urban Aeronautics ilitangaza kwamba ndege yake isiyo na rubani – ambayo iliundwa kwa matumizi ya kijeshi – ingeanza kutumika kufikia 2020, lakini sana katika uokoaji.

Usalama ni kitu muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Je, unadhani teknolojia ya ndege zinazojiendesha zenyewe zitapunguza ajali za angani? Na je, ukipewa nafasi ya kupanda drone utathubutu?

Chanzo: BBC

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com